DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Wanakera sana mkuu, tumekuwa taifa la udaku udaku tu na mambo yasiyo na msingi kuanzia viongoz wakuu mpaka kwetu huku. Wenzetu Kenya wanapiga hatua za maana aisee sijui nani katuletea hiki kituko.
Waliotuibia kura na wao wanajuta, wamejikuta walituwekea rais mshamba sana.
 
Hivi Magufuli si ndo anashtumiwa kumbeba Makonda?
Tuna ushahidi wa kutosha wa marais waliofanya madudu ya kuwabeba ndugu na marafiki kwenye mizigo yao pale bandarini, je Magufuli angekuwa anambeba Makonda ,si angetuma memo tu?? Kwamba hayo makontena yaachiwe Mara moja?

Ninahisi Magufuli hajawahi kumbeba Makonda, ila hapendi kushinikizwa kuchukua hatua,

Naanza kupata mwanga wa mambo mbali mbali

Magufuli hajawahi kumbeba Makonda, si ambebe hata kwa hili??

Au kambeba kaona habebeki? Au kambeba kaona amechoka, au hajawahi kumbeba kabisa
Jiulize kama tukio hili angekuwa amelifanya let say RC wa pwani hapo tusiende mbali, leo hii angekuwa ameshasahau kama alikuwa RC, kigugumizi hiki ni ujumbe tosha kuwa DAB bado anabebwa, japo siku zake zipo karibu mno kutenguliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote hao wanajuana mie naona kama vile mpango mkakati wa kumtoa commissioner wa kodi ya forodha kwenye reli. Mwisho wasiku ule upande pendwa utashinda.
 
Kuna watu wapo duniani kama bendera hawajahi tumia japo punje ya ubongo wao kwasababu ya mahaba.

1. Yale makontena yamebeba viti vya ofisini wala si madawati, Niambieni ni shule gani wanakalia viti vya kuzunguka?
2. Uagizwaji Wa makontena haukuzingatia taratibu, niambieni tangu lini msamaha umeanza kutolewa kwa huruma ya walengwa?
3. Kwanini mwenye Makontena aliyakana pale mwanzo?
4. Yakiachwa yapite Bure Tutakuwa tumewafundisha nini Wasimamizi Wa forodha na ushuru kwa vitu visivyo zingatia utaratibu?
5. Kwanini yaliandikwa jina la Makonda (Personal)?
===============
NOTE; Mtoto hata ukimkalisha kiti cha mwalimu Mkuu haina maana ndiyo atajua kusoma na kuandika
Uteuz na utenguz mpaka wikiend; kuwa na subira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi sasa sakata la makontena ya Makonda limefikia patamu, baada ya Musiba kutamka wazi kuwa angekuwa na mamlaka yeye angeyachukua jumla na siyo kuyapiga mnada!

Amempongeza waziri wa fedha Dr Mpango kwa kusimamia sheria na kubainisha kuwa nchi ina mihimili mitatu na inafanya kazi bila kuingiliwa!

Hivyo amemtaka Makonda kulipa kodi ya hayo makontena, ambapo inaelezwa kuwa makontena hayo yamebeba samani za ofisi za shule lakini kwa nyepesi nyepesi ni kuwa kilichopo ndani ni samani za hotel na viti na meza chache za ofisi zilizowekwa kama geresha tu.

Amesema makontena hayo ni zaidi ya 800...!

Ngoja huu mtanange tuuone Musiba Vs Makonda.

Napita tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya lile sakata la makontena kati ya mkuu wa mkoa wa Dar na waziri wa fedha,wananchi kila kona walisema,na wakatabiri Makonda kufutwa kazi lakini mpaka dakika hii bado hajafutwa kazi na anaendelea kuwa mkuu wa mkoa

Siku za hivi karibuni Makonda amelaumiwa na Rais hadharani kuwa mkoa wake umeshuka kimapato na madiwani wanalipana posho mara mbili hata hivyo Rais hakuona sababu za kumuondoa nafasi hiyo kwa kosa tajwa

Wangekuwa watendaji au viongozi wengine wamefanya makosa mfululizo wangekuwa wameisha tumbuliwa zamani na wananchi wangekuwa wamesahau lakini kwa Makonda ni tofauti ,kumbuka kisa cha DED Bukoba ,kusahau kiasi cha fedha tu akatumbuliwa sembuse Makonda anapambana na serikali yake mwenyewe lakini hatumbuliwi

Sababu hizi hapa

Ishu ya Makonda kupambana na madawa ya kulevya ilimfanya awe na maadui kila kona na hata kuongezewa ulinzi na serikali

Inafahamika duniani ukishaingia katika harakati za kupambana na madawa ya kulevya basi maisha yako huwa yapo hatarini hivyo Rais anaona dhahiri kuwa akimfuta Makonda kazi basi atakuwa amewapa tiketi ya kuuawa kwa Makonda

Sio siri tena Makonda ana maadui kila kona baada ya sakata la madawa hivyo Rais anamhurumia sana

Ni swali la kujiuliza baada ya Magufuli kumaliza muda wake na Rais mwingine akaingia madarakani na asipomteua makonda kuendelea kuwa mkuu wa kitengo fulani ili aendelee kulindwa je,atakimbia nchi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora hata nisingesoma wala kucoment Uzi huu wa kiwango cha vumbi
 
Ktk historia ya Tanzania Luna Raisi alinyonga watu wengi lkn mpaka leo anashirikiana na watu kwa uwazi bila mitutu kumzunguka.Kwetu hatufikia kwa kina Escobar na mtu aliyefsnys jambo LA haki uoga unakuwa mdogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbukeni mnatolea matamko kwenye mkoa wake alishasema akiamua anakufukuza mkoani kwake soon tutawaona dodoma
 
Back
Top Bottom