DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

View attachment 848681

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

View attachment 848680

Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.

Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
Laana ya aliyelaaniwa ina nguvu kweli? Mzimu wa Warioba unafanya kazi.
 
Hakuna aliye juu ya sheria kama alitumika kumg'oa nape safari hii amegonga mwamba atakwenda yeye na vitisho vyake!

Kitendo cha Dr. Mpango kijitokeza kujibu hadharani mambo ya magazetini yamenifanya nithibitishe ile shaka yangu kwamba hii ni sinema ili kuhadaa umma kwamba kila mtu analipa kodi. Hayo makontena hayana lolote la maana zaidi ya kutafuta political millage. Waziri mzima unajibu maelezo ya gazetini tena kwa maneno ya mwenzako aliyeko serekali!?

Huyo Makonda ndio amekuwa akijinasibu kila mtu afanye siasa kwenye jimbo/mkoa wake. Ilifikia mahali akasema hakuna waraka kwenye mkoa wake. Iweje leo akatolee vitisho nje ya mkoa wake na serekali ijitokeze hadharani kujibu matamko yake? Hilo movie wachezewe wenye upeo mdogo.
 
Ok. Naona picha linaanza.
Lakini muda mwingine tutumie busara zaidi kuliko nguvu na sheria. Kodi ya serikali inayodaiwa ni 1.2bn, ina maana hayo makontena yanathamani zaidi ya hiyo let say 3bn. Serikali inauza kontena moja kwa 60mn ili ipate pesa yake. Katika hiyo 1.2bn zitatumika katika bajeti kununulia tena hivyo vifaa vya ofisi za walimu, ambavyo vinaweza visifike wingi huo. So, nionavyo mimi, serikali ndio itakayo poteza kwa kuingia gharama kwa vitu ambavyo wamepewa bure. Pili, inawavunja nguvu hata jamaa waliochangia wakiombwa tena. Ndio maana naona inahitajika busara coz wote tunajenga nyumba moja kasoro njia tunazo tumia. Na upuuzi kama huu nilishawahi kuuona pale MOI, walitangaza mnada wa kuuza vitanda vya wagonjwa wakati palepale muhimbili kuna watu wanalala chini sababu ni taasisi tofauti japo zipo chini ya wizara moja.
Tanzania kichwa cha mwendawazimu hadi kwenye uongozi sio mpira tu.
Na kama sio kichwa cha mwendawazimu basi vigogo wa Dawa za kulevya wana nguvu ya kutisha. RC tokea alipovianza adui ni wengi sana. Nimestuka Mhe. Waziri hadharani unarejerea vyombo vya Habari kuleta malumbano na mteule mwenzako?
 
Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

View attachment 848681

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

View attachment 848680

Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.

Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
Dr. Mpango ni akili kubwa sana.
Anajua matatizo yatakayokuja kumkuta baadae endapo atakiuka sheria na kutoa msamaha kwa mizigo inayotakiwa kulipia kodi. Kama makontena hayo yameingia kwa jina la mtu binafsi ni lazima yalipiwe kodi ili kuwa fundisho kwa wengine. Isije ikatokea mtu au kiongozi wa serikali au chama cha siasa siku moja akaingiza kontena la mabomu kwa kutumia jina binafsi. Sheria ifuate mkondo wake bila kusita.
Misamaha ya kodi inayotolewa ikinyume cha sheria imewagharimu mawaziri wengi wa Fedha hata baada ya awamu za wateuzi wao kuisha.

...Hongera sana DR. Mpango Umeona mbali sana
 
Ni jambo la aibu kabisa kwa watendaji wa serikali moja, chama kimoja, wameteuliwa na rais mmoja, wanalumbana wazi wazi kama watoto wasio na adabu.

Jambo hili linaonesha udhaifu wa serikali yetu, haifanyi maamuzi kwa pamoja na kuzingatia "collective responsibility".

Kila mtu anafanya maamuzi kivyake.

Na panapotokea mgongano, viongozi hawana ukomavu wa kuongea na kumaliza tofauti zao kwenye vikao vya ndani.

Wanagombana kwenye vyombo vya habari kama wendawazimu.

Hapo, kitu cha kwanza kabisa, sijali nani yuko sawa na nani kakosea, kule kulumbana hivi tu, kunawafanya wote wawe wamekosea.

Kama viongozi wakubwa kabisa wa serikali wanatoa mfano huu, watoto wa shule ya msingi wanajifunza nini hapo?
Kweli hata Mimi nashangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amelaaniwa yeye aliyemupiga WARIOBA amabaye ni sawa na babu yake
Shame on him
 
Na kama sio kichwa cha mwendawazimu basi vigogo wa Dawa za kulevya wana nguvu ya kutisha. RC tokea alipovianza adui ni wengi sana. Nimestuka Mhe. Waziri hadharani unarejerea vyombo vya Habari kuleta malumbano na mteule mwenzako?

Kwa hyo waziri yeye asitekeleze wajibu wake alioapia kuutekeleza kisa kichwa kilichojaa ubongo wa madafu yeye ruksa kuropoka.acheni upunguani katika kilaza hawezi kushindana na phd, nepi alimwambia MANENO ALIYOONGEA NI YA KISAYANSI NA MTU MWENYE ELIMU YA KUUNGA UNGA HAWEZI KUMUELEWA sembuse, mfyuuuuu
 
Back
Top Bottom