Diason David
JF-Expert Member
- Aug 2, 2018
- 7,557
- 7,367
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Laana ya aliyelaaniwa ina nguvu kweli? Mzimu wa Warioba unafanya kazi.Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.
View attachment 848681
Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.
"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.
Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.
"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango
Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.
Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.
"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango
View attachment 848680
Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.
Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.
Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
Ila sidhani unakumbuka ile ya rugweUtenguzi wa Paul Makonda is Loading....
Hata wewe.....kweli nimeamini vijana wa pole pole ni vipeperushi mnabadilika kulingana na upepo hata mfalme kuna siku mtamkanaHakuna aliye juu ya sheria kama alitumika kumg'oa nape safari hii amegonga mwamba atakwenda yeye na vitisho vyake!
Hakuna aliye juu ya sheria kama alitumika kumg'oa nape safari hii amegonga mwamba atakwenda yeye na vitisho vyake!
Na kama sio kichwa cha mwendawazimu basi vigogo wa Dawa za kulevya wana nguvu ya kutisha. RC tokea alipovianza adui ni wengi sana. Nimestuka Mhe. Waziri hadharani unarejerea vyombo vya Habari kuleta malumbano na mteule mwenzako?Ok. Naona picha linaanza.
Lakini muda mwingine tutumie busara zaidi kuliko nguvu na sheria. Kodi ya serikali inayodaiwa ni 1.2bn, ina maana hayo makontena yanathamani zaidi ya hiyo let say 3bn. Serikali inauza kontena moja kwa 60mn ili ipate pesa yake. Katika hiyo 1.2bn zitatumika katika bajeti kununulia tena hivyo vifaa vya ofisi za walimu, ambavyo vinaweza visifike wingi huo. So, nionavyo mimi, serikali ndio itakayo poteza kwa kuingia gharama kwa vitu ambavyo wamepewa bure. Pili, inawavunja nguvu hata jamaa waliochangia wakiombwa tena. Ndio maana naona inahitajika busara coz wote tunajenga nyumba moja kasoro njia tunazo tumia. Na upuuzi kama huu nilishawahi kuuona pale MOI, walitangaza mnada wa kuuza vitanda vya wagonjwa wakati palepale muhimbili kuna watu wanalala chini sababu ni taasisi tofauti japo zipo chini ya wizara moja.
Tanzania kichwa cha mwendawazimu hadi kwenye uongozi sio mpira tu.
Mkuu vipi kwa mtazamo wako hapo nani yupo sahihi? Makonda au waziri?
Sent using Jamii Forums mobile app
Dr. Mpango ni akili kubwa sana.Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.
View attachment 848681
Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.
"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.
Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.
"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango
Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.
Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.
"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango
View attachment 848680
Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.
Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.
Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.
Kweli hata Mimi nashangaaNi jambo la aibu kabisa kwa watendaji wa serikali moja, chama kimoja, wameteuliwa na rais mmoja, wanalumbana wazi wazi kama watoto wasio na adabu.
Jambo hili linaonesha udhaifu wa serikali yetu, haifanyi maamuzi kwa pamoja na kuzingatia "collective responsibility".
Kila mtu anafanya maamuzi kivyake.
Na panapotokea mgongano, viongozi hawana ukomavu wa kuongea na kumaliza tofauti zao kwenye vikao vya ndani.
Wanagombana kwenye vyombo vya habari kama wendawazimu.
Hapo, kitu cha kwanza kabisa, sijali nani yuko sawa na nani kakosea, kule kulumbana hivi tu, kunawafanya wote wawe wamekosea.
Kama viongozi wakubwa kabisa wa serikali wanatoa mfano huu, watoto wa shule ya msingi wanajifunza nini hapo?
Kweli tutajua mbeleniSerikali yetu inapenda sana Isidingo.
Ila huu mchezo wanaocheza wameshapanga kila kitu...
Wanajua kabisa nini kinaendelea na lini kitaisha.
Na albadiriLaana ya aliyelaaniwa ina nguvu kweli? Mzimu wa Warioba unafanya kazi.
Na kama sio kichwa cha mwendawazimu basi vigogo wa Dawa za kulevya wana nguvu ya kutisha. RC tokea alipovianza adui ni wengi sana. Nimestuka Mhe. Waziri hadharani unarejerea vyombo vya Habari kuleta malumbano na mteule mwenzako?
Umeonaeeeeee?Hata wewe.....kweli nimeamini vijana wa pole pole ni vipeperushi mnabadilika kulingana na upepo hata mfalme kuna siku mtamkana