fundinaizer
JF-Expert Member
- Dec 15, 2016
- 1,758
- 2,713
Umekosea mkuu,maoni yako yamekaa vizuri ila hapo kwa Mpango umekosea,.. hamtaji Makonda kwenye media ila anahalalisha watu wakanunue hayo makontena baada ya mkwara wa DAB kuwa watakaothubutu kununua watalaaniwa, jaribu kufuatlilia alichoongea Mipango.Akishaanza kuongelea habari za kwamba amesikitishwa na vitisho vya Mkuu wa Mkoa tayari kashajiingiza katika malumbano na Mkuu wa Mkoa na wananchi tunaoelewa "collective responsibility" katika serikali ni nini, tunaona wote wanakosea.
Bashite kakosea kwenye kosa la msingi la kujifanya yeye ni special case anatakiwa kuwa treated kwa sheria ya peke yake, Mpango kakoseakuendekeza malumbano ya kumtaja Mkuu wa Mkoa na positions zake through the media in public.
Ni vile tupo katika zamaambazo kazi za serikali hazina heshima tu, lakiniingekuwa zama za uongozi wa kujiheshimu, hapo Waziri hata kama anahimiza watu waje kununua, asingeongelea habari za Mkuu wa Mkoa, au angesema tu "ofisi yangu inawasiliana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuzungumza zaidi, lakini kwa sasa huu ni manada halali na wananchi msiwe na hofu"
Sent using Jamii Forums mobile app