DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

DAR: Licha ya RC Makonda kusema atakayenunua Makontena yake atapata laana kali, Waziri Mpango aagiza yapigwe mnada

Brother... tayari fanicha ziko bandarini. Walimu hawana fanicha.
Misaada mingapi ya mahindi inakuja toka Marekani inapita bila kodi wakati kuna mahindi Iringa, Katavi na Ruvuma yanaharibika?

Tukiamua kuijenga nchi tuijenge. Tukiamua kufuata sheria sawa tutakuwa sawa pia. Ila suuala je tunapiga hatua au tunarejea nyuma?
...Coming together is a beginning; keeping together is progress; working together is success...
Kaazi Kweli kweli..Alipovamia Clouds na mitutu ungeandika hizi nyaraka pia ningekuelewa! Hivi mnafikiri Mpango alienda bandarini na kuongea yale from nowhere?

Mpango sio Nape..
 
Exactly!
But wait unaposema diaspora tuchange kwa chochote alichoagiza makonda whether ni kupitia shirika or so, does she seems that loyal? I’ll never ever eva eva everrrrr changa kwa anything that has makonda name in it, once mwizi tapeli mwongo na muuaji, he will always be. Rather nikampangishie nyumba omba omba aliekaa barabarani hata kama kwa uongo, kama hela inaniwasha sana.
[emoji23][emoji23][emoji23] I was just giving an easy way out. Makonda should get creative now to acquire the merchandise, people got money, he got friends i think, or else everybody is waiting for him to fall face flat on the floor. Either way he gotta be creative.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiboko yenu mzee wa msoga.mlikamata Mali za mkewe.akawanyoosha.sijui na yeye alifata hyo sheria mnayosemaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi siongei ushabiki mkuu, wala situmii hisia, makonda kakosea 100%, kapiga shortcut, Sheria ikianza kumhukumu unalalamika nini, unajua iliwekwa kuzuia nini, ukitaka kujibu usitumie hisia nipe logic mkuu, mi siongei ushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo yako yote yamekaa kisiasa zaidi.Ukisoma kwa makini utagundua hilo na wala haliitaji elimu.Nikuulize ni nchi gani iliyofanikiwa bila kufuata sheria za nchi ikiwa pamoja na katiba iliweza kuendelea.?.Mpango yuko sahihi kabisa maana anafuata sheria zilizotungwa na bunge na mkuu wa mkoa anafuata sheria ili kuweza kutawala mkoa wake;Kwanza tukumbushane kwa mala ya kwanza yalipoulizwa kwamba makontena ni ya nani majibu yalitoka yapi alipoulizwa makonda.Kwa jibu alilolitoa linaonyesha dhahiri sio kusudio unalolitoa sasa hivi kwamba ni kwa ajili ya vifaa vya shule na walimu.Kama ni zawadi kutoka marekani sheria inasemaje ya maadili ya umma.Majibu unayo ila kufanya watanzania kwa kuwaita masikini na wajinga kitu ambacho sio sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Benny Mwaipaja, WFM - Dar es Salaam

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

View attachment 848681

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! Unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwanini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! Si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

View attachment 848680

Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diaspora nchini Marekani.

Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.

Hiyo ndiyo serikali..hakuna double standard hapa. Safi sn Mh. Mpango
 
Sheria si mnatunga wenyewe na kuzipitisha kwa kusema ndioooo!!Sasa hapo unashangaa nini?!

Alafu jiulize ni kwanini mwanzoni aliakana alafu baadae akayakubali?

We jua tu hilo ni dili limebumbuluka.
Sio hivyo tuu, kwanini yaje kwa jina lake?? Na sio walengwa?? Alisha zowea deal sasa ime buma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23] I was just giving an easy way out. Makonda should get creative now to acquire the merchandise, people got money, he got friends i think, or else everybody is waiting for him to fall face flat on the floor. Either way he gotta be creative.

Sent using Jamii Forums mobile app

He should understand now how much people hates him. Siku akitumbuliwa watu watapiga vigelegele. I, being one of them. Kabebwa vya kutosha akiepuka hili basi Tz sio ya kuishi hata kwa kujaribu tena!
 
He should understand now how much people hates him. Siku akitumbuliwa watu watapiga vigelegele. I, being one of them. Kabebwa vya kutosha akiepuka hili basi Tz sio ya kuishi hata kwa kujaribu tena!
Ila ukija kukuta yameshatolewa kwa msamaha wa raisi usijinyonge [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheria ni za Ccm walitunga wao nakuitia ndio hadi hapa tulipofika wametufikisha wao
 
Back
Top Bottom