Hao wenye elimu kubwa si ndio hao waliokuwa wanabuni miradi ya upigaji kama EPA,, ESCROW na uchafu mwingine wa aina hiyo!!?.
Hao wenye shule za maana si ndio hao ambao wanaendesha ma-vogue na magari ya milioni 400 wakati Mama zao vijijini wanajisaidia haja kubwa maporoni pembeni ya nyoka na chatu!!?.
Hao wenye shule nzuri si ndio hawa walioua mashirika makubwa mpaka yakawa yanashindwa kutoa gawio serikali kuu!!.
Hizi ndizo akili za mtanzania halisi, anajivunia elimu wakati hakuna cha maana ambacho elimu yake inaisaidia nchi hii.
Huyu dogo anaweza kuwa na matatizo yake binafsi lakini hizi juhudi za kuwatafutia waalimu furnitures, hizi juhudi za kusaidia kinamama wanaotelekezewa watoto, ni lazima Mungu atazilipa. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.