Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

Dar: Maandamano ya ACT Wazalendo kuelekea Ikulu kushinikiza waliotajwa wizi kwenye ripoti ya CAG kuchukuliwa hatua

Maandamano makubwa yameanza eneo la Fire Kariakoo yakiwa yameandaliwa na ACT-Wazalendo kushinikiza wezi wote walionaswa na Ripoti ya CAG waondolke maofisini kwenda magerezani.

Maandamano yanaongozwa na viongozi waandamizi wa chama hicho Cha upinzani na yataishia lango Kuu la Ikulu ya Magogoni ili yapokelewe na Rais Samia Suluhu Hassan.

Binafsi Niko mbele na bango langu. Hali ya hewa si rafiki sana hata kuandika ni taabu lakini umma unazidi kujitokeza kuwataja wezi wakamatwe. Karibuni.
Wamuache mama afanye kazi hayo maandamano hayana tija NAMWOMBA ndugu yetu MZALENDO ZZK
Amwache mama afanye Kaz maandamano hayana tija Kwa Sasa......

Nashaur jeshi la police litumie NGUVU zake kuwabzibiti na kuwasweka ndani Ili wamwache Mama Samia afanye kazi bila presha za wanasiasa uchwara.....

Mimi Huwa nafikiria badala vyama vyetu vya siasa viachane na siasa za majitaka na propaganda uchwara Kwa mwamvuli wa democrasia....

Ni muda Sasa CCM na vyama vingine kujitafakari sanaaa ni wakati sasa tupate mwarobaini wa kutibu matatizo yetu ya tangu Uhuru sio Kwa maandamano hayana tija....
 
Acha uongo, tangu lini upinzani wameongoza nchi hii. Mna hasira na upinzani walioko nje lakini CCM inayowaibia kila siku mnailamba matakao na kuisujudia. Ondoa unafiki wako hapa.
Ccm na Upinzani Jambo ni moja tu ..ccm ni wezi na Upinzani nao ni mulemule tu .Nchi inakuwa na Upinzani usiokuwa na dira .Tabia za kupenda kuitisha press ni za utoto.
 
ACT kinapambana sana kuwa chama kikuu cha upinzani. Wakiendelea hivi chini ya miaka mitatu ijayo watakuwa wameshaipiku CHADEMA hasa hii ya sasa.

Maandamano yana nia nzuri sana sema mwamko wa Watanzania ndiyo zero....

View attachment 2591675
Chama hakikuwi kirahisi hivyo, lazima uwe na mtandao mpana nchi nzima. Mbowe aliutengeneza kuanzia 2004 mpaka 2014 so sio rahisi sana mwingine kufikia hapo. ACT kama sio Maalim kujiunga kingekua kipo Ujiji tu
 
Wapinzani wa Tz hawana ushirikiano baina yao.

econonist zitto junior JokaKuu Bams
Tatizo ni itikadi hazifanani, mfano ACT wanaamini ujamaa ila Chadema tunaamini katika ubepari wa soko huria. Pia ACT ni mrengo wa kushoto ila Chadema ni mrengo wa kati-kulia so ni wahafidhina Sasa unadhani tutaiva chungu kimoja na wajamaa wa kidemokrasia wa ACT?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hivi ACT wana vijana kweli ata wa kuandamana?

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
Hali ngumu mkuu bahasha inahusika,+hela ya vocha...

mtu mwenye akili timamu, uache Kazi Yako uandamane bure!? Tenachama chenyewe ACT!?

Huwa wanatoa sana njuruku ACT...ni kujisogeza tu Kwa viongozi wao wa karibu walioko kwenye mfumo
 
Hili ndilo tatizo kubwa zaidi Tanzania kuliko hata ufisadi...Ingetakiwa woote tuandamane hayo ya kuangalia nan kaandaa maandamano ni ya baadae...Nnaamini tungeleta mshtuko mkubwa Serikalini lakin kwa kujigawa huku ndo tushapoteza kabiiiisaaaaa
Mkuu tatizo kubwa lililopo vyama vya upunzani haviaminiani. Na hii inatokana na vyama vingine kuonekana vipo vipo tu, havina mwelekeo wa upinzani makini kwa lengo la kuchukua madaraka kupikia Uchagu Mkuu. Suala la kila chama kufanya mandamano kivyake vyake ndio udhaifu mkubwa katika kuwaunganisha Wananchi.
Maandamano haya kwanza yange ratibiwa wa viongozi Wakuu wa Vyama vyote vya upinzani na ndipo wange utangazia Umaa wa Watanzania na sio Wanachana wa Vyama ili kuhalalisha 'LENGO" la maandamano kuwa ni la Kitaifa zaidi. Kwa kufanya hivyo ndipo tungepata jibu la kwa nini maandamano haya pewi umuhimu hapo TZ.
 
Hili ndilo tatizo kubwa zaidi Tanzania kuliko hata ufisadi...Ingetakiwa woote tuandamane hayo ya kuangalia nan kaandaa maandamano ni ya baadae...Nnaamini tungeleta mshtuko mkubwa Serikalini lakin kwa kujigawa huku ndo tushapoteza kabiiiisaaaaa
Mkuu, tatizo kubwa lililopo ni kwamba vyama vya upunzani haviaminiani. Na hii inatokana na vyama vingine kuonekana vipo vipo tu, havina mwelekeo wa upinzani makini kwa lengo la kuchukua madaraka kupitia Uchaguzi Mkuu. Suala la kila chama kufanya mandamano kivyake vyake ndio udhaifu mkubwa sana katika kuwaunganisha Wananchi.
Maandamano haya kwanza yange ratibiwa wa viongozi Wakuu wa Vyama vyote vya upinzani na ndipo wange utangazia Umaa wa Watanzania na sio Wanachana wa Vyama, ili kuhalalisha 'LENGO" la maandamano hayo kuwa ni mandamano la Kitaifa zaidi. Kwa kufanya hivyo, ni dhahiri Umaa wa Watanzania unge ona ama kutambua kuwa ni maandamano ya Umaa na hivyo kushiriki ama kutoshiriki; hapo ndipo tungepata jibu la kwa nini maandamano hapa Tanzania hayapewi umuhimu unaositahili.
 
Katika hali inayoonyesha wananchi kukerwa na Ufisadi nchini, chama cha ACT Wazalendo kimefanya maandamano jijini Dar es salaam, kuonyesha kukerwa na ukithiri wa Ufisadi nchini.

ACT Wazalendo wanaeleza kuwa ripoti iliyotolewa na CAG imeonyesha kuwa hii nchi Inaliwa kulia, Kushoto, Juu, katikati na kila sehemu.

Miongoni mwa malengo ya maandamano hayo ni Kumtaka Rais Samia achukue hatua kuwawajibisha wezi ba mafisadi badala ya kutoa kauli lainilaini tu zisizosaidia lolote kukomesha nchi kutafunwa kama biskuti.

Wakati huohuo Polisi wameingilia kati kuzuia maandamano hayo yaliyokuwa yakielekea Ikulu Dar salaam kumtaka Rais achangamke kupambana na ufisadi asijivutevute!

Hapa Chini ni Polisi wakiwa na Magari yao ya Deraya wakiwazuia wananchi kutimiza haki yao ta kikatiba kuandamana kuonyesha kukerwa na Ufisadi nchini.

 
Wamuache mama afanye kazi hayo maandamano hayana tija NAMWOMBA ndugu yetu MZALENDO ZZK
Amwache mama afanye Kaz maandamano hayana tija Kwa Sasa......

Nashaur jeshi la police litumie NGUVU zake kuwabzibiti na kuwasweka ndani Ili wamwache Mama Samia afanye kazi bila presha za wanasiasa uchwara.....

Mimi Huwa nafikiria badala vyama vyetu vya siasa viachane na siasa za majitaka na propaganda uchwara Kwa mwamvuli wa democrasia....

Ni muda Sasa CCM na vyama vingine kujitafakari sanaaa ni wakati sasa tupate mwarobaini wa kutibu matatizo yetu ya tangu Uhuru sio Kwa maandamano hayana tija....
Tukiwa na watu sampuli Yako robo ya idadi yetu nchi hii itaondolewa kwenye ramani ya Dunia. Wewe ni mjinga sana. Afanye kazi Gani zaidi ya kupambana na mafisadi.
 
Tukiwa na watu sampuli Yako robo ya idadi yetu nchi hii itaondolewa kwenye ramani ya Dunia. Wewe ni mjinga sana. Afanye kazi Gani zaidi ya kupambana na mafisadi.
Kila mtu akijiamulia awe ana enda Ikulu magogoni kama anaenda sebuleni kwake....

Ume ambiwa mambo Yana shuhurikiwa so mnajifanya mna uchungu na hili taifa kuliko mtu yeyote.....

Watu wa USALAMA wanajua na wanaelewa....

IF YOU USE THIS ENERGY FOR YOUR LIFE, THEN YOU WILL NOT BE BEGGING FOR FOOD

🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Wasalaam
Kwa Sasa
+267
 
Tuko pamoja.

CHADEMA wananiangusha sana ckuiz, yaani kauli Ile ya Mnyika alivyotoa ndo kimya Hadi Leo.

Kama Bado mnaandaa, wananchi tunaeaunga mkono act Kwa muda.

Mnyika naye angenyamaza. Alitakiwa akishasema vile, baada ya siku anatangaza maandamano nchi nzima. Shida pale juu, Hakuna mhamashishaji. Nadhani maridhiano uchwara yamewafunga wasiongee Sana.
 
Mkuu kwani huoni au hujui kuwa CHADEMA na CCM wameungana sasaivi wote adui yao ni mmoja hayati Magufuli?

Hapana sio kweli mkuu. CHADEMA Wana justification ya kumsema Magufuli maana aliwashughulikia kwa mambo mengi, ila kusema kwamba CCM na CHADEMA wote wezi, labda Kama watakuwa wameingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Kama Zenji au serikali ya mseto.
 
Maandamano yameruhusiwa, mbona CDM wameandamana Hadi wamechokwa wenyewe bila bugudha?

Ukimya wa CDM ktk hili sababu wanazijua viongozi.

Maandamano ya kwenda kwenye mkutano sio maandamano per se Bali matemebezi. Ila maandamano ya kutaka spika aondeoke au bunge lijadili kwa dharura ripoti ya CAG Hapo ndipo utajua Kama maandamano yameruhusiwa.
 
Wewe na Tindo ni miongoni mwa wahafidhina msioridhishwa na uongozi wa Mbowe hapo Cdm, ila kumbukeni mchango wa Mbowe kwa Cdm unahusika pakubwa kwenye kukifanya hichi chama kuwa chama kikuu cha upinzani.
Bams zitto junior

No mkuu, Mbowe namheshimu Sana, yeye ndio alinifanya niingie chadema mwaka 2000, baada ya yeye kushinda ubunge Hai. Lakini, kwenye kasoro lazima tusema. Mbowe kwa Sasa anakitoa CHADEMA kwenye misingi yake na kukifanya Kama mshirika wa CCM, amabayo sio afya kwa CHADEMA.

Ndio maana mpaka ACT wanapata guts za kufanya maandamano ila sisi CHADEMA tumefungwa miguu na maridhiano uchwara ambayo hayana impacts yoyote. Nakuambia kwa haya maridhiano uchwara, hata CHAUMMA itaipiga kibesi serikali Ila sisi tutabakia kimya.
 
Back
Top Bottom