Dar: Mashehe washauri wanaomkashfu mitandaoni ‘Nabii Mkuu’, Dkt. Geor Davie wa Gurumo ya Upako, kumfata Arusha kwa nauli yao

correct
 
Hao mashehe wana matatizo ya kimsingi.
Watamteteaje mtu ambaye amethibitika kutenganisha ndoa ya mtu na mke wake?
Kama wakitaka wamslimishe ili awe mwislamu.
 
Mashehe uchwara walioamua kumtumikia Binadamu mwenzao badala ya kumtumikia Mungu.
Imani dhaifu na nina uhakika sio Waislamu hao, wala hawajui wanalolifanya zaidi ya kuhongwa

Njaa mbaya sana ila hii imezidi na hali ya sasa wala siwashangai wanafiki hao na moto ndio sehemu yao
 
Sheikh kasema wamemwona nabii anasaidia watu kwa maombezi na kuwasaidia watu moja kwa moja. Kilichowavutia masheikh ni hiyo ya pili ya kusaidia watu moja kwa moja wakiamini hawataenda na kurudi tupu.
 
Hii nchi hiii,tutaona Mengi!,kule watu Wana galagala kumpokea Raisi!,UDSM wanampa heshima kwamba kakuza uchumi,wakati kitaa hari ni tete!!sasa hii ndio komesha,mashekh wamsifu "nabii"wa kikristo!!??hata sijaelewa Kuna game gani hapa Propagandist wa ccm wanataka kucheza!!?
Hivi mnajua hata Idi amini alipewa PHD ya heshima?
 

Attachments

  • 20221203_141127.jpg
    58.4 KB · Views: 9
Nasikia nabii huyo wa Arusha hajambo mifukoni, imenikumbusha wale mashekhe, manabii na mitume waliokuwa kila siku wanaamkia kwa mwendazake ikulu kuvizia bahasha.
HILI NALO NI TANGAZO.
 
waumini waislamu tu ndio wanijibu!
Kwa mujibu wa quran, hadith, na miratul rasul nani ni hatma nabii??
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] vijana muwe na adabu basi. Hao ni wazee wetu. Tanzania tunaheshimiana na tunaishi kiuungwana na kwa udugu wa kupigiwa mfano. Hebu acheni kuendekeza hoja za kibinafsi.

Hakuna shida kwa masheikh kumtetea mchungaji huo ni upendo wa next level. Msijisahaulishe namna wachungaji na makanisa yalisimama na watanzania wengine kutetea masheikh wa uamsho kuachiwa huru ingawa walikuwa na itikadi za kibinafsi. Tuwe na utu kwanza.
 
Huu ni ushahidi kuwa kampeni ya 'nabii' inaelekea anapopataka.

Nabii anataka awapiku wenzake wote, kina wa upako, Mwapesa, Kakobe na wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…