balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 16,841
- 15,673
Au tuseme Alex angejaribu upande wa provocation Kama utetezi wake! Je, Gift alifanya nini na aliongea nini dhidi ya Alex? Je,alichofanya kinakidhi vigezo vya kuwa provocation?Kwenye kesi ya Jamuhuri dhidi ya Said Mwamwindi,provocation ilikataliwa ingawa mkuu wa mkoa komred Kleruu alithibitika kumfanyia dharau na uchokozi mtuhumiwa na ndipo mtuhumiwa alipofuata bunduki na kumlima marehemu.Sifahamu mahakama ingeliwekaje suala la Alex kutoa bastola yake mara kadhaa na kuombwa airudishe mahala pake na kisha yeye kuomba msamaha.Je,mahakama ingeamua vipi kama tabia hiyo aliyoionesha mtuhumiwa ingeonekana kuendana na sheria ya ushahidi ya Tanzania yaani TEA kifungu cha kumi kinachoeleza kuhusu maandalizi ambayo mtuhumiwa huyafanya kabla hajatenda jinai?