Dar: Meli yenye magari 3,743 yawasili bandarini ikitokea Japan

Wakumbuke tu gas iliyopo Mtwara haiitaji passport kwenda nchi nyingine. Kijiografia tupo jirani na Mozambique. Inawezekana tunashare gas deposits wakati sisi tunajishauri wenzetu wanainyonya tu. Tukija kushtuka mzigo umekata tayari...
 
Hahaha sasa hiyo nayo ni meli kubwa? Kakutane na kina Ever Ace huko hiyo utaiona ni kamtumbwi.
 
Duh ndinga zinaingia kwa wingi sana. Tutegemee foleni njiani kama yote yatabaki bongo

UCHUMI WA KATI unatamalaki
 
Nakumbuka wakati tukiwa shule msingi tulifanya tour ya kwenda bandarini, aisee tulikuta meli zimeleta mafuta, mkuu meli ni kubwa sana.
Siku moja nitaenda kutalii bandarini, nione hizo meli zinavyofanana, kwa kweli sikuwahi kufikiri kama meli inaweza kubeba magari mengi kiasi hicho
 
Toka juzi mtandao wao wa kupata invoice haufunguki huwezi kulipa ili utoe mzigo. Utendaji ni mbovu sana wanahitaji mabadiliko
 
Pongezi kwa bandari.
sasa tunategemea mapato ya serikali yataongezeka mara dufu.
 
Hapo 80% ya hayo magari yanabaki Dar es Salaam mengine machache ndiyo yanaenda mikoani na sehemu zingine [emoji119][emoji119]
 
Toka juzi mtandao wao wa kupata invoice haufunguki huwezi kulipa ili utoe mzigo. Utendaji ni mbovu sana wanahitaji mabadiliko
Kabisa mkuu nimeingiza Trucks tokea ijumaa kupakia Plant tokea jumatatu nikuzungushana tu machine mbovu wanakosa hata betri za ku boost machne kweli? aibu sana mtu akiwa nnje hawezi kuamini tukisemacho.
 
Wakati tukifurahia kuletewa magari 3000 ya kununua tukumbuke haya
. Magari ni mitumba hivyo yana athari zake kimazingira
. Tunaenda kuimarisha uchumi wa wenzetu kunzia hayo magari mpaka vipuri
Badala ya kufurahia mitumba toka Japan ni bora wangekuja na option ya kujenga viwanda vya ku assemble hayo magari
 
Hapo 80% ya hayo magari yanabaki Dar es Salaam mengine machache ndiyo yanaenda mikoani na sehemu zingine [emoji119][emoji119]
Mkuu umeelewa walivyosema 65% ya magari yaliyoshushwa ni Transit?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…