Huwa mara nyingi sana nayatilia shaka maelezo ya Polisi kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu nchini, hasa yale ambayo polisi huwa wanahusika, kwa mfano kuuwawa kwa watuhumiwa. Siku zote nimeamini kwamba Polisi wanaweka chumvi nyingi sana katika kusimulia hayo matokio, na hata mara nyingine kupindisha ukweli kimakusudi kwa faida au maslahi ya serikali au ya polisi wenyewe.
Sasa katika kile ambacho kinaonekana ni muendelezo wa Polisi kusimulia mambo tofauti na tukio, ni hili la utekwaji wa MO. Huwezi kuamini kwamba wanasimulia juu ya tukio lilelile. Dereva wa Uba ambaye alikuwapo wakati wa tukio la utekaji anaeleza ifuatavyo;
Sasa, tofauti na hayo maelezo ya dereva wa Uba ambaye alikuwapo, Mambosasa ambaye hakuwapo kwenye tukio anaeleza yafuatyo;
Sasa wana JF, hebu niambieni, tuamini maelezo yepi; ya dereva wa Uba aliyekuwapo wakati tukio likitokea, au Mambosasa ambaye anaweza akawa na ajenda nyingine kwenye kutoa haya maelezo kama ilivyo kawaida ya Polisi?
Ukweli ni kwamba binafsi naona kama Mambosasa anatoa maelezo kwa namna ya kupotosha ukweli fulani. Utafikiri ana wasiwasi hawa watu wasiojulikana ni wale wanaojulikana na anajaribu kufanya watu wasidhani kwamba watekaji ni watu wasiojulikana wanaojulikana ili serikali isilaumike.
Lakini jumuisho la yote ni kwamba tunafurahi kusikia MO ameshapatikana.