Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Nimemsikiliza Kamanda Mambosasa anadai kuwa ametekwa na Wageni kwa vile ni wazungu!! ........... Hivi kwani hakuna Wazungu watanzania!!?

Anyway, kama walikuwa wameficha usoni hivi kweli kwa tukio la haraka kama utekaji utawatofautishaje wazungu, wahindi au waarabu!!
Itakua ni MZUNGU KICHAA
 
Alianza zakaria hatukuambiwa kwanini ilitokea vile.haya mo tena julizeni watekaji wanataka nini na nani.wanateka ili iweje
Ongeza na yule mmriki wa super sami alie okotwe kwenye kiroba
 
Huwa mara nyingi sana nayatilia shaka maelezo ya Polisi kuhusu matukio mbalimbali ya uhalifu nchini, hasa yale ambayo polisi huwa wanahusika, kwa mfano kuuwawa kwa watuhumiwa. Siku zote nimeamini kwamba Polisi wanaweka chumvi nyingi sana katika kusimulia hayo matokio, na hata mara nyingine kupindisha ukweli kimakusudi kwa faida au maslahi ya serikali au ya polisi wenyewe.

Sasa katika kile ambacho kinaonekana ni muendelezo wa Polisi kusimulia mambo tofauti na tukio, ni hili la utekwaji wa MO. Huwezi kuamini kwamba wanasimulia juu ya tukio lilelile. Dereva wa Uba ambaye alikuwapo wakati wa tukio la utekaji anaeleza ifuatavyo;

1539244477108.png

Sasa, tofauti na hayo maelezo ya dereva wa Uba ambaye alikuwapo, Mambosasa ambaye hakuwapo kwenye tukio anaeleza yafuatyo;

1539244584433.png

Sasa wana JF, hebu niambieni, tuamini maelezo yepi; ya dereva wa Uba aliyekuwapo wakati tukio likitokea, au Mambosasa ambaye anaweza akawa na ajenda nyingine kwenye kutoa haya maelezo kama ilivyo kawaida ya Polisi?

Ukweli ni kwamba binafsi naona kama Mambosasa anatoa maelezo kwa namna ya kupotosha ukweli fulani. Utafikiri ana wasiwasi hawa watu wasiojulikana ni wale wanaojulikana na anajaribu kufanya watu wasidhani kwamba watekaji ni watu wasiojulikana wanaojulikana ili serikali isilaumike.

Lakini jumuisho la yote ni kwamba tunafurahi kusikia MO ameshapatikana.
 
mbona kuna taarifa makonda kakanusha kuwa kapatikana mbona watu wanacheza na akili za watu
 
According to Mr. Mambosasa, three people have been arrested in connection to the incident. The police said all entry points around airports and other exit points have been closed.

Nilidhani kuimarisha ulinzi ingetosha!
Kwahiyo taratibu za kusafiri Leo kutoka Dar ni hamna au?
Can't understand this!
Hakuna kusafiri leo[emoji15] [emoji15] ...what the heck?
 
According to Mr. Mambosasa, three people have been arrested in connection to the incident. The police said all entry points around airports and other exit points have been closed.

Nilidhani kuimarisha ulinzi ingetosha!
Kwahiyo taratibu za kusafiri Leo kutoka Dar ni hamna au?
Can't understand this!
mkuu hayo ni machache kati ya mengi yanayozid kuja kaa tayari
 
Back
Top Bottom