Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Haya matukio ya kutekana yanaichafulia jina Tz yetu na yasipodhibitiwa yataathiri utalii na uwekezaji
 

taswira ya taifa kweli imechafuka vibaya sana kwa tukio hili vyombo vya habari vya kimataifa vyote vinaongelea

kutekwa kwa MO Hii kitu inatutia doa kama nchi kisiasa na kiuchumi na kiusalama.
 
Nadhani burning issue leo ingekua mwendo kasi ila ndio ivyo tena

Hivi habari ya mwendokasi ndio imekufa? Mmmmm hapa kuna jambo. Yaani kila matukio makubwa ya kuitingisha Dar yakitokea, basi hupandikizwa tatizo jingine ili watu wasahau matatizo ya msingi.

Hizi mbinu sijui zitaisha lini, maana hii ya mwendo kasi ni bonge ya tatizo, ni balaaaaa.

Haya tuone haya matatizo mawili yatakwendaje sambamba.
 

Hamna kitu km iko,,serikali imteke MO wakati ndio wakuza uchumi wetu,,hii coment yako mkuu itakuletea matatizo
 
UPDATE 4: 1100HRS
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekanusha taarifa za kupatikana kwa mfanyabishara Mohammed Dewji, na kwamba taarifa zilizosambaa kuwa amepatikana sio sahihi.
Nimemsikiliza vizuri Makonda ........ amesema kuwa "Majibu sahihi ni kuwa Mo amepatikana na wahalifu wametiwa mikononi mwa vyombo vyetu vya dola...."

Kama siyo kweli basi AIBU KUBWA ............ Kiongozi Mkubwa kama yeye hakutakiwa kutoa habari zisizo na uhakika!!
 
Itakuwa ni bashite tu anataka kuwakamua hela ndugu za Mo na kumlazimisha Mo ahamishe fedha kwenda akaunti za bashite za offshore.

Hapa muhimu ni kucheza na akaunti zake ikionekana kunafanyika muamala kwa njia ya mtandao ,fasta wana block,then wanafanya tracking kujua hao jamaa wapo sehemu gani..

Hapa ndiyo vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ,vinapaswa kuonyesha weledi wa hali ya juu katika hili sakata


Mwenyezi Mungu amsimamie Mo dhidi ya hao wahalifu.
 
Ushauri mzuri Hapo kwenye INTERPOL/FBI ili apatikane haraka akiwa hajadhurika.. Ajabu watakataa kuonyesha wanaweza hata wakishindwa.
hapo mwishoni umeongea ukweli mchungu.
 
Dawa yao ni kuwapiga au kuwapiga Risasi kama yule Zakaria wa huko Tarime.
Zakaria aliusoma mchezo wote akachukua hatua. Ndugu yetu Mo Dewji yeye hakujua alishtukia tu hawa.
 
Hamna kitu km iko,,serikali imteke MO wakati ndio wakuza uchumi wetu,,hii coment yako mkuu itakuletea matatizo
serikali inayo ongozwa na kichaa unadhani unaweza kuliona hilo kama ambavyo wewe umeliona "...? Mbona mnalazimisha chizi aweze kuwa na Akili timamu ""?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…