Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Inamaana alikua hana ulinzi hadi atekwe kiurahisi namna hiyo?
 
Mbona unaongea pumba ktk jambo serious
Nchi ya matukio ya kuwasahaulisha watanzania juu ya matumizi mabaya ya pesa zao wanazolipa kodi kutumika vibaya kuwanunua wapinzani kurudia chaguzi kwa gharama kubwa huku huduma za kijamii zikizidi kudorola, wanatengeneza Matukio ili watanzania wasahau vingi vioja wanavyofanyiwa na CCM kwa sasa.
 
Hakuna hapo kuna mchezo unachezwa. Haiingii akilini kuwa ametekwa, huenda kuna mpango unafanywa juu ya mtu fulani, I'll ikitokea watu tujue aaah kawaida, mbona MO nae alitekwa!! Lakini hakuna siri chini ya jua kila kitu kitakuwa peupe muda sio mrefu. La tatu kwanini MO anaishi maisha ya aina hiyo? Hivi kweli yeye hajijui kuwa na Tycoon, au anazani kuishi hivyo ndio kutamfanya apendwe? Lazima aamue kuishi tofauti kabisa, tena tofauti sana. Haiwezekanj MO akashindwa kuwa na fitness Center kwenye kasri lake, ok hana. Basi haiwezekani akawa hana bodyguard anapotoka ndani ya viunga vya kasri lake, jamani MO ni nembo ya taiga letu.
Natoa angalizo kwa wanaofanya huu mchezo, wanaliangamiza taifa. Wasidhanie ni suala dogo, hakuna wawekezaji watakaokuja Tanzania kuwekeza na hata wakija watakuja vibaraka wao.
Ni nani aneapanga ujinga huu, na kwanini wanamchekea? Baba wa Taifa alisema, ukizoea kula nyama ya watu, hautaacha. Wamezoea kuwateka akina Ben Sanane, Dr Ulimboka na wengine kuwaua kabisa, sasa dhambi inatamalaki wameanza kutekena wenyewe kwa wenyewe. Amini nakuambia kila kitu kitakuwa wazi, huenda wamemtaka kwa kumtisha ili aisaidie kifedha jamii , taasisi au kikundi cha watu fulani itajulikana. Sitaki kwenda mbali sana, ila anaepanga huu mchezo, lazima akamatwe ashtakiwe na kufungwa. Labda tu kama kuna baraka ya Mungu. Acha tu niingie mtaani kutafuta riziki ya kila siku.
Wasiojulikana waliokwenda kumpiga Risasi Tundu lisu kule Dodoma sasa wanajulikana lakini hakuna aliyewachukulia hatua, mbinu pekee iliyosalia ni kuwasomea Alibadiri kubwa tena ikasomewe mbali huko Somalia kwa siri kubwa ili kuepuka kutibuliwa na yule shehe wa mkoa wa Dsm rafiki yake Le mutuz na Bashite.
 
Hapa kuna fukuto tena la kivita kama mieleka ngoja tukae pembeni tuombe na kusali kuna jambo kubwa la siri kama zilivyo siri nyingine
 
Ndo nashangaa, kwann asiwe na gym ya home kwake, wakati hapa dar kuna matajiri wadogo ambao wanamiliki private gym home kwao, ubahili mwingine una-cost, itakuwa maybe ametekwa na kikundi cha majambazi kinachotaka pesa ili aachiwe, au kama katekwa na wanasiasa, bhasi itakuwa hajui kuishi kinafiki na wanasiasa, Mengi anajua kuishi kinafiki na wanasiasa ndo maana hatekwi. Mama Sabrina Mshana Jr
Watu wanapoamua kukudaka haijalishi uko wapi watakupata kumbuka mtu wa level ya MO kumrukia sio issue ndogo unaweza kuunga dot watu hao wanatoa wapi ujasiri
 
Back
Top Bottom