Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Dar: Mfanyabiashara Mohamed Dewji(Mo Dewji) atekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay

Nimemsikiliza Kamanda Mambosasa anadai kuwa ametekwa na Wageni kwa vile ni wazungu!! ........... Hivi kwani hakuna Wazungu watanzania!!?

Anyway, kama walikuwa wameficha usoni hivi kweli kwa tukio la haraka kama utekaji utawatofautishaje wazungu, wahindi au waarabu!!
Acha kuumiza bichwa lako jua kua mtengenezaji wa hii movie hajawahi kufanikiwa jambo
 
Kuna hizi habari kwamba Mfanyabiashara Mohamed Dewji ametekwa leo asubuhi maeneo ya Collosium Gym , Oysterbay alipokuwa ameenda kufanya mazoezi..

Mwenye habari kamili atujuze.

======

UPDATES:

Mfanyabiashara maarufu nchini, ambaye pia ni mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji (Mo Dewji), anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto, saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11. Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro athibitisha.

RPC Lazaro Mambosasa amesema Polisi Dar inafuatilia madai ya kutekwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu nchini

UPDATE 1:

Dereva wa Uber amesema aliona watu 4 wakishuka kwenye gari dogo, wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu na kumchukua Mohammed Dewji

UPDATE 2:

RPC Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili. Aidha, amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa Mo Dewji

UPDATE 3:

RPC Lazaro Mambosasa amesema watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano kuhusu kutekwa kwa mfanyabiashara Mo Dewji

Moderator update taarifa iliyotolewa na mambosasa kuwa amepatikana
 
Cha nsingi apatikane hayo mambo yao mengine watajijua wao sie tumeshakubali kuishi kama tuishivyo mambo ya kushtuana na kuumizana mioyo hatutaki
 
Yeah ulisema nakumbuka
U see its my faithful nilijua hilo....mimi huwa sipendi kupanik katika matukio yoyote makubwa huwa najipa matumaini ila yakipita masaa 24 hapo lazima niwe na wasiwasi na ndiyo nitaanza kuumia moyo,nakumbuka msiba wa mshua naletewa taarifa sikuamini baada ya muda kama masaa matatu nasikia kwenye vyombo vya habari sijakaa sawa naona watu wanakuja shule naitwa ba mwalimu mkuu dah hapo muda huo nilianza kupaniki[emoji17]
 
Kwa jinsi alivyopatikana fasta...

Naji-convince itakua ishu ilisukwa na Bash.ite kujenga kiki watu wasikomalie sana mwendokasi!

Hao suspects zijui kama watatuonesha....!

Sanaa mtindo mmoja!

Only in awamu ya 5 ndio utapata habari hizi na nyingine za kijinga kama kuvamia vituo vya TV!
hajapatikana, lkn hisia zangu zinamhisi Bashite...anisamehe kama ninakosea
 
Back
Top Bottom