Dar Mpya: Mawaziri na wabunge wako nyuma ya Umoja Party. Wengi watiifu kwa hayati Magufuli

Dar Mpya: Mawaziri na wabunge wako nyuma ya Umoja Party. Wengi watiifu kwa hayati Magufuli

CCM ina mizizi mirefu mno, CCM wanalindwa na Dola, CCM wana nguvu ya msajili wa vyama, CCM wanalindwa na mkurugenzi wa uchaguzi, CCM wamefanikiwa kupandikiza woga kwa watanzania WOTE! Hivyo hata kije chama gani, bure tu!

Tena chama kinachotoka ndani yake. Watakifuta kabla halijaanza kazi.
 
Kuna genge ndani ya CCM linatajwa kuunda Umoja Party kuendeleza Umagufuli Tanzania, sasa kati ya vitu muhimu ambavyo Magufuli anakumbukwa navyo ni kuzuia vyma vya siasa kujieneza kwa kupiga marufuku mikutano yao pamoja na sheria kali za vyama

Magufuli mara nyingi alisikika akisema CCM itatawala milele na alichukulia wanaoikosoa CCM kama ni wahaini wasiotakiwa kuonewa huruma, Umoja Party hawaoni watakuwa wanasaliti maono ya Magufuli?

pia watashinda vipi uchaguzi? Magufuli alianzisha ujtaratibu wa kuchagua makada wa CCM kuwa Wakurugenzi ambao ndio watakuwa wanasimamia uchaguzi na kutangaza matakoeo, na kamwe hawatatangaza mtu wa upinzani labda CCM yenyewe iamue kuwaachia, je Umoja Party watashinda vipi hata kiti kimoja cha ubunge kwa misingi hii ya Magufuli?


Kuanzisha chama cha upinzni kumuenzi Magufuli ni usaliti mkubwa kwa Magufuli ambaye alikuwa akiona upinzani ni maadui

Bora uwaambie ukweli hawajitambui wanataka nini.
 
Sasa wanakuwaje watiifu wa mtu ambaye amekufa tayari?

Yani inawezekanaje ukawa mtiifu wa Nyerere wakati hazungumzi🤭
 
Alifariki tena akiwa CHADEMA

Hapana Mpendazoe alihama Chadema na kurudi CCM baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 na kuanza kuiponda Chadema akitegemea uteuzi ila ndiyo hivyo akaachwa mpaka leo. Tena alifanya vibaya maana Chadema walijitoa wakampa nafasi ya kugombea ubunge kishapu huku wanachadema wakiwa hawamtaki lakini mwishowe akawasaliti na kurudi CCM.
 
Hili suala la kukataa katiba mpya na mfumo mpya kabisa wa utawala Tanzania limewaliza wanasiasa wengi na bado litaendelea kuliza wengine. Ni suala la muda, na ni kundi gani liko jikoni tu. Lowassa baada ya kutemwa na CCM alikiona cha mtema kuni na akabaki kulialia wakati alikuwa na uwezo wa kubadilisha mfumo kabla. Haya, Magufuli naye alipokuwa jikoni, timu Msoga na kina Kinana walikuwa wanalialia. Likatokea lililotokea na sasa wako jikoni, gemu limegeukia kwa timu mwendazake. Na timu Samia nayo isipokubali kuleta mabadiliko ni jambo la muda tu wanaweza kujikuta kwenye wakati mgumu kuliko makundi mengine yote yaliyopita.
Wameshajifunza.. Hili kundi la Samia kulitoa madarakani labda jeshi liingilie kati.
Kwa sasa CCM watakua makini sana kumchagua mgombea, hakuna Magufuli mwingine atakayetokea
 
Watu hawatii marehemu wanatii falsafa zake za uongozi. Kwa kuwa yeye ndo alianzisha aina hiyo ya uongozi watu sasa wanapitia kivuli chake kujipambanua/kujinadi Kwa jamii.
Falsafa ya Magufuli ni zipi?
 
Si mtiifu wa marehemu. Ni watiifu Kwa maono aliyoyaamini marehemu. Matendo MAZURI ya mtu HAYAFI kamwe. Mf Hadi Leo Mandela anatajwa Afrika nzima Kwa aliyoyatenda.

Magufuli ana matendo gani mema? Kuuwa na kutukana watu?. Kujenga madaraka na reli ilikiwa kwenye mpango wa miaka mitano wa serikali sio maono yake.
 
NDOTO YANGU YA ALFAJIRI

..Ninasikia nyimbo za mapambio kwa mbaaali sana.. ghafla ninawaona Chadema na ACT wakitangulia mbele na msalaba, mashada ya maua. Sanduku lina rangi mbili likiwa limebebwa kwa UMOJA wakielekea malaloni. Ninajaribu kusogelea kwa karibu ninakuta ndio wanamalizia shughuli ya kupumzisha mwili.

Mwisho ninayasikia maneno haya toka kwa waombolezaji

"Vita umeipigana, pumziko la milele liwe nawe"

Bwana ametoa, wana ametwaa

Ninashtuka toka usingizini ninaangalia saa yangu inasoma saa 10 alfajiri, tar 20 April 2022. Ninakwenda kuhakikisha kama nilifunga mlango vizuri ninakunywa maji ninarudi tena kulala.

Muulize Membe alidhani kuchukua madaraka Ni kazi nyepesi akaishia kupata kura elfu tisini. Mtu ambaye aliiyingisha CCM Ni Lowassa tu wengine Ni wafa maji. Hicho chama kimepewa karipio kwamba kimeanza harakati bado hakijasajiliwa.
 
Nawaona mawaziri waandamizi 3 wapo
"Mstaafu' wa mhimili mmojawapo yupo
Wabunge hasa wa kanda ziwa wapo!
Anyway, ni watu wasio na mvuto ktk jamii hivyo hawana madhara yoyote.
 
UP imeshaanza kuwapa pumzi ya moto

UP kitu gani. Waulize Moto wa ACT ulivyokuwa kipindi kile, halafu wakambulia kura 90,000 za urais na mbunge mmoja. Watanzania wasikie tu. Vyama ni viwili tu, CCM na CHADEMA.
 
Muulize Membe alidhani kuchukua madaraka Ni kazi nyepesi akaishia kupata kura elfu tisini. Mtu ambaye aliiyingisha CCM Ni Lowassa tu wengine Ni wafa maji. Hicho chama kimepewa karipio kwamba kimeanza harakati bado hakijasajiliwa.
Hujui lolote wewe!
Uliza Lissu CCM wakuambie namna walivyomchakachua kwa wizi wa kutisha!
Uliza Mrema alichowafanyia CCM 1995 ndio utajua wizi wa CCM!
 
Back
Top Bottom