Kuna genge ndani ya CCM linatajwa kuunda Umoja Party kuendeleza Umagufuli Tanzania, sasa kati ya vitu muhimu ambavyo Magufuli anakumbukwa navyo ni kuzuia vyma vya siasa kujieneza kwa kupiga marufuku mikutano yao pamoja na sheria kali za vyama
Magufuli mara nyingi alisikika akisema CCM itatawala milele na alichukulia wanaoikosoa CCM kama ni wahaini wasiotakiwa kuonewa huruma, Umoja Party hawaoni watakuwa wanasaliti maono ya Magufuli?
pia watashinda vipi uchaguzi? Magufuli alianzisha ujtaratibu wa kuchagua makada wa CCM kuwa Wakurugenzi ambao ndio watakuwa wanasimamia uchaguzi na kutangaza matakoeo, na kamwe hawatatangaza mtu wa upinzani labda CCM yenyewe iamue kuwaachia, je Umoja Party watashinda vipi hata kiti kimoja cha ubunge kwa misingi hii ya Magufuli?
Kuanzisha chama cha upinzni kumuenzi Magufuli ni usaliti mkubwa kwa Magufuli ambaye alikuwa akiona upinzani ni maadui