Dar Mpya: Mawaziri na wabunge wako nyuma ya Umoja Party. Wengi watiifu kwa hayati Magufuli

CCM ina mizizi mirefu mno, CCM wanalindwa na Dola, CCM wana nguvu ya msajili wa vyama, CCM wanalindwa na mkurugenzi wa uchaguzi, CCM wamefanikiwa kupandikiza woga kwa watanzania WOTE! Hivyo hata kije chama gani, bure tu!

Tena chama kinachotoka ndani yake. Watakifuta kabla halijaanza kazi.
 

Bora uwaambie ukweli hawajitambui wanataka nini.
 
Hahahaaa!! Wanamtii Marehemu? Ambae hawajui yuko kuzimu au motoni.
 
Sasa wanakuwaje watiifu wa mtu ambaye amekufa tayari?

Yani inawezekanaje ukawa mtiifu wa Nyerere wakati hazungumzi🤭
 
Alifariki tena akiwa CHADEMA

Hapana Mpendazoe alihama Chadema na kurudi CCM baada ya uchaguzi mkuu wa 2015 na kuanza kuiponda Chadema akitegemea uteuzi ila ndiyo hivyo akaachwa mpaka leo. Tena alifanya vibaya maana Chadema walijitoa wakampa nafasi ya kugombea ubunge kishapu huku wanachadema wakiwa hawamtaki lakini mwishowe akawasaliti na kurudi CCM.
 
Wameshajifunza.. Hili kundi la Samia kulitoa madarakani labda jeshi liingilie kati.
Kwa sasa CCM watakua makini sana kumchagua mgombea, hakuna Magufuli mwingine atakayetokea
 
Watu hawatii marehemu wanatii falsafa zake za uongozi. Kwa kuwa yeye ndo alianzisha aina hiyo ya uongozi watu sasa wanapitia kivuli chake kujipambanua/kujinadi Kwa jamii.
Falsafa ya Magufuli ni zipi?
 
Si mtiifu wa marehemu. Ni watiifu Kwa maono aliyoyaamini marehemu. Matendo MAZURI ya mtu HAYAFI kamwe. Mf Hadi Leo Mandela anatajwa Afrika nzima Kwa aliyoyatenda.

Magufuli ana matendo gani mema? Kuuwa na kutukana watu?. Kujenga madaraka na reli ilikiwa kwenye mpango wa miaka mitano wa serikali sio maono yake.
 

Muulize Membe alidhani kuchukua madaraka Ni kazi nyepesi akaishia kupata kura elfu tisini. Mtu ambaye aliiyingisha CCM Ni Lowassa tu wengine Ni wafa maji. Hicho chama kimepewa karipio kwamba kimeanza harakati bado hakijasajiliwa.
 
Nawaona mawaziri waandamizi 3 wapo
"Mstaafu' wa mhimili mmojawapo yupo
Wabunge hasa wa kanda ziwa wapo!
Anyway, ni watu wasio na mvuto ktk jamii hivyo hawana madhara yoyote.
 
UP imeshaanza kuwapa pumzi ya moto

UP kitu gani. Waulize Moto wa ACT ulivyokuwa kipindi kile, halafu wakambulia kura 90,000 za urais na mbunge mmoja. Watanzania wasikie tu. Vyama ni viwili tu, CCM na CHADEMA.
 
Muulize Membe alidhani kuchukua madaraka Ni kazi nyepesi akaishia kupata kura elfu tisini. Mtu ambaye aliiyingisha CCM Ni Lowassa tu wengine Ni wafa maji. Hicho chama kimepewa karipio kwamba kimeanza harakati bado hakijasajiliwa.
Hujui lolote wewe!
Uliza Lissu CCM wakuambie namna walivyomchakachua kwa wizi wa kutisha!
Uliza Mrema alichowafanyia CCM 1995 ndio utajua wizi wa CCM!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…