Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Blandina1.jpeg
blandina 2.jpg

Mtangazaji wa kituo cha ITV cha jijini DAR ES SALAAM Bi Blandina Sembu amekutwa akiwa ameuawa maeneo ya ITV Mwenge usiku saa sita.

Mwili huo ulitambuliwa na Henry Mabumo aliyekuwa mtangazaji mwenzake kabla Mabumo hajahamia TBC.

Mwili ulichukuliwa na Polisi usiku huohuo.
Taarifa rasmi zitafuata.

=====

Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limethibitisha taarifa za kifo cha mtangazaji wa ITV Blandina Sembu, likieleza kuwa ni tukio la mauaji.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Ramadhan Kingai ameeleza kuwa walipata taarifa za mwili wa Blandina kutupwa mbele ya baa ya Maryland saa tano usiku.

Amesema gari aina ya Toyota Noah ilifika katika eneo hilo na kusimama kwa muda mfupi kabla ya kutupa mwili wa Blandina akiwa tayari amefariki.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa bodaboda waliokuwa wamepaki jirani na eneo hilo walishuhudia gari lililowashaa taa likisimama kwa dakika mbili kisha wakaona mwanamke ametupwa.

“Uchunguzi unaendelea ila tulichobaini huyu mtu hakuuliwa pale, mauaji yalifanyika sehemu nyingine pale walienda kumtupa.

“Amekutwa na majeraha usoni yanayoashiria alikuwa akijaribu kupambana kujitetea na hata jicho lake linaonekana alipigwa na kitu kizito,” amesema.

Kamanda huyo ameeleza kuwa makachero wa jeshi hilo wanaendelea na uchunguzi na muda si mrefu watawafikia waliotekeleza mauaji hayo.
 
Back
Top Bottom