Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

Dar: Mtangazaji wa ITV, Blandina Sembu atupwa barabarani kituo cha Mwenge ITV akiwa ameuawa

Pitia uzi kwa utulivu, mleta mada kaendelea kufafanua kwamba Mabumo walikuwa Bar ya jirani na hapo mwili ulipotupwa, so walivyosikia makelele ya bodaboda wakaja mbio kuona na Mabumo anamfahamu maana walikuwa wote ITV...
Alikua anakunywa karib na alipookotwa sawa nimeelewa
 
IMG_20210328_143729.jpg

Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni limethibitisha kutupwa kwa mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari ITV/Radio one Blandina Sembu katika eneo la njia panda ya ITV na watu wasiojulikana waliokuwa wakitumia gari aina ya Noah.
 

Mtangazaji wa kituo cha ITV cha jijini DAR ES SALAAM Bi Blandina Sembu amekutwa akiwa ameuawa maeneo ya ITV Mwenge usiku saa sita.

Mwili huo ulitambuliwa na Henry Mabumo aliyekuwa mtangazaji mwenzake kabla Mabumo hajahamia TBC.

Mwili ulichukuliwa na Polisi usiku huohuo.
Taarifa rasmi zitafuata.

=====

Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni limethibitisha taarifa za kifo cha mtangazaji wa ITV Blandina Sembu, likieleza kuwa ni tukio la mauaji.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Ramadhan Kingai ameeleza kuwa walipata taarifa za mwili wa Blandina kutupwa mbele ya baa ya Maryland saa tano usiku.

Amesema gari aina ya Toyota Noah ilifika katika eneo hilo na kusimama kwa muda mfupi kabla ya kutupa mwili wa Blandina akiwa tayari amefariki.

Kamanda Kingai ameeleza kuwa bodaboda waliokuwa wamepaki jirani na eneo hilo walishuhudia gari lililowashaa taa likisimama kwa dakika mbili kisha wakaona mwanamke ametupwa.

“Uchunguzi unaendelea ila tulichobaini huyu mtu hakuuliwa pale, mauaji yalifanyika sehemu nyingine pale walienda kumtupa.
Amewakosea nini ?
 
sijui ni nini(ningekuwa mpiga ramli au mganga ) inangesema ni maswala ya kimapenzi sidhani kama ni kazi .
nilipenda vipindi vyake japo wanawake wenyewe walikuwa wanapishana navyo wanasubiri isidingo
 
Back
Top Bottom