Wakuu huko kijijin nilikokulia, kuna kisa kimoja cha jamaa jambazi. Naogopa kukiweka humu kwa sababu 2.
1 Nikisimulia kama kisa kilivyo watu wanaweza kunijua. Labda nitumie codes.
2 Naamini wengi watadhani ni stori ya kutunga (chai)
Kwa ufupi ni hivi, huyu jamaa alikuwa mshirikina hatari alikuwa na machale ya ajabu sana. Ukimwendea kiroho safi unamkuta tu vzr, ukiwa na nia mbaya anapotea kimiuijiza.
Yule mjinga, alisumbua sana zaidi ya mwaka Polisi wanahaha huku na kule. Amini usiamini..Ili polisi wamkamate libidi washirikiane na wazeee waingie kwenye ushirikina.
walichokifanya kwanza waliua machale yake. Siku ya kumkamata walimkuta bar akila maisha na crew yake. Walipofika wakamchapa na lile jani la mgomba la kati kati (lile changa ambalo bado limejikunja) halafu wakamvisha (wakapitisha) kichwani underskirt. Hapo hakuwa na ujanja wowote. Alikamatwa kama kuku. Yule jamaa alipata taabu sana...yaan aliteswa zaidi ya Yesu. Wiki nzima yupo kituoni ni kichapo..kichapo kipondo. Baadae walimmaliza hata hawakupeleka mahakamani. Mpaka wanamuua, alikuwa hana baadhi ya viungo vya mwili. vidole, masikio, minofu ya baadhi ya maeneo ya mwili n.k maana alikuwa anakatwa analazimishwa kula nyama zake.
Mpaka anakamatwa alikuwa ameua watu wengi sana huyu mwamba.
Hapo ni 1990s to less than 2001