ASILI YA WAPALESTINA KUTOUNGWA MKONO, PIA KUOGOPWA SANA NA MATAIFA YA KIARABU
Dr Edward SAID professor wa chuo cha The College de France jijini Paris Ufaransa, mpalestina aliyewasili miaka ya 1950 katika jiji hili tajwa la ulaya Magharibi
View: https://m.youtube.com/watch?v=7g1ooTNkMQ4
Akiwa na kiu ya kujiendeleza kimasomo baada ya kuwasili akiwa kijana asiye na certificate wala diploma yoyote amezaliwa 1935 katika familia tajiri hivyo kusomeshwa shule nzuri na baadaye kwenda ngambo kusoma katika vyuo tajwa duniani nchini Marekani vya Princeton na Harvard kisha kuwa professor University of Columbia New York US.
Akiwa ngambo masomoni alizungukwa na marafiki wengi wa karibu wa kimagharibi na kiyahudi pia ingawa nje ya kundi hilo alionekana kama adui mkubwa kwa kukumbatia ugaidi wa wapalestina.
Wazazi wake Prof. Edward Said yaani mama yake alizaliwa Nazareth huku baba mzaliwa wa Jerusalem. Baadaye wazazi wake walihamia Lebanon na kuwa raia wa huko Lebanon ingawa vyeti vyao vinaonesha walizaliwa Palestine nchini Israel.
Prof. Edward Said mpalestina mkristo anaendelea kuelezea uaina wa watu waliozaliwa eneo hilo la Mashariki ya Kati wenye mchanganyiko mwingi wa kihistoria, kijamii na muingiliano wa mataifa mengi kutokana na mambo mengi yaliyojitokeza.
Prof. Edward Said katika maandiko yake kuhusu mtizamo wa Magharibi kuhusu Mashariki uwe katika vitabu, michoro, picha, simulizi, aina ya fikra za Mashariki kuwa yanafanana na kuweza kuiva katika chungu kimoja bila kutibua ladha ni mtizamo usio onesha hali halisi.
Prof. Edward Said anasema mwenyeji wa Egypt ana tabia tofauti na sema mwenyeji wa Syria vile vile wa kutoka Jordan wana mtizamo tofauti na wa kutoka Tunisia au Saudia.
Prof. Edward Said katika mihadhara yake na uandishi umeleta malumbano mengi moto na kuvutia wengi kusikiliza pia kusoma.
Prof. Edward Said kuhusu kuwepo vitabu vingi vya jiografia na historia vipya ambavyo vimejaribu kufuta ya zamani na kuandika vitu vingi vipya kwa sababu maalumu zenye manufaa kwa ....
Prof. Edward Said anaikumbuka Beirut ya miaka 1970s na 1980s iliyowakaribisha kwa mikono miwili siyo wapalestina tu bali waarabu kutoka nchi za Egypt, Syria, Jordan, Iraq, Sudan n.k wote walikimbilia Beirut Lebanon lakini baadaye wote walifurushwa kutokana na majeshi ya mgambo ya wenyeji wa KiShiite na Kikristo kuwazunguka na kuwatimua
Na baada ya hapo hasahasa wapalestina hawatakiwi tena katika mataifa ya kiarabu kufuatia nchi zilizowapa ukimbizi kwa wingi kama Jordan na Lebanon kuwaona wapalestina ni wakorofi na wakiwa wakimbizi huamua kujiingiza ktk siasa za wenyeji wao.
Mataifa ya kiarabu kuingia woga kwa imani ya Wapalestina kwenda mbali zaidi kuchukua upande wa moja wa wenyeji wao na kushiriki kwa kutumia silaha kujaribu kupindua serikali za wenyeji wao.
Kwa wapalestina kuamini itapatikana serikali mpya ya kiarabu iliyo majimuni Pan Arabian itakayounga mkono, harakati ya umoja mpya wa Kiarabu kuishambilia Israel, na ifutike ili wapalestina warudi ktk nchi wanayoamini yakwao pekee siyo ya mataifa mawili ya Palestine na Israel yanayoishi sambamba kwa kutambua uwepo wa mataifa mawili kiasili ....