Dar: Polisi yazima maandamano, yakiri kumshikiliwa Sheikh Ponda kwa mahojiano

Dar: Polisi yazima maandamano, yakiri kumshikiliwa Sheikh Ponda kwa mahojiano

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP. Muliro amepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika leo Novemba 10, 2023 Dar es Salaam, pia amewatahadharisha wananchi kutoshiriki maandamano hayo.

=====

Polisi Dar wazima maandamano, Sheikh Ponda akamatwa
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limezima maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika kuanzia viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Manzese, huku likikamata baadhi ya viongozi wanaodaiwa kuyandaa akiwemo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Taarifa za maandamano hayo inayoandikwa kuwa imetolewa na Shura ya Maimamu Tanzania, zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii leo Novemba 10, zikieleza kuwa ni maandamano ya kutetea Mamlaka ya Palestina ambayo yalipangwa kufanyika leo saa 7:30 mchana kuanzia Mnazimmoja hadi Manzese.

Kufuatia taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Muliro alitoa taarifa kupitia video kwenye mitandao ya jamii akipiga marufuku maandamano hayo.

Mwananchi Digital ilifika Mnazimmoja na kukuta umati wa watu, huku askari Polisi wenye sare wakiwa wameimarisha ulinzi kuzunguka viwanja hivyo.
Chanzo: Mwananchi

===========

UPDATES: TAARIFA YA JESHI LA POLISI

Akizungumza na JamiiForums kuhusu taarifa hiyo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Jumanne Muliro amesema:

"Tulimueleza taarifa zinazohusiana na mikutano au makusanyiko, taarifa zake anatakiwa kupeleka kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya kwa mujibu wa Katiba na Sheria, na Mkuu wa Polisi wa Wilaya anatakiwa kutoa mwongozo wa kiusalama, yeye (Ponda) hakufanya hivyo.

"Baada ya kuelezwa hivyo, hakufanya chochote, akawa anahamasisha kwenye mitandao kuhusu, akaanza kukusanya watu, hakufuata utaratibu kama anakubaliwa au la.

"Kinachofanyika anahojiwa, tunataka kujua kuna nini kinachoendelea kuhusu mipango iliyopo.

"Baadaye tutaangalia mazingira, tutaangalia hiki kinachochunguzwa kama kinadhaminika au tofauti, baada ya mahojiano tutaangalia dhamana kwa mujibu wa Sheria na anatoa ushirikiano mzuri katika mahojiano."
Maandamano ya kuunga mkono Palestina yakiruhusiwa, kumbuka kuna wengine wanaunga mkono Israel, sasa hii nchi patakuwa hapatoshi, Polisi wasiruhusu kabisa hiyo habari!
 
Maandamano ya kuunga mkono Palestina yakiruhusiwa, kumbuka kuna wengine wanaunga mkono Israel, sasa hii nchi patakuwa hapatoshi, Polisi wasiruhusu kabisa hiyo habari!
Wakiristo mlivyokuwa woga wa kufa. Kama si waislam uhuru wa Tanganyika ungalipatikana 2023 labda
 
Maandamano ya kuunga mkono Palestina yakiruhusiwa, kumbuka kuna wengine wanaunga mkono Israel, sasa hii nchi patakuwa hapatoshi, Polisi wasiruhusu kabisa hiyo habari!
Badala ya kuandama kushinikiza wabadhirifu wa kodi zetu wabananishwe wanaandamana kwa mambo yasiyotuhusu. Huu ni upumbavu
 
Wakiristo mlivyokuwa woga wa kufa. Kama si waislam uhuru wa Tanganyika ungalipatikana 2023 labda
Wewe wacha ngebe umeshafakamia mchemsho wa nguruwe huko unajambajamba tu huku. Kula chuma hicho
JamiiForums-105152417.jpg
 
Kumbe mwamba anafakamia huyo mdudu..
Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
8 na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
Bible
 
Mbona wewe unakula na gongo unakunywa? Wacha unafiq
 
Back
Top Bottom