Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

Wewe ni mtumishi wa umma hujui hustling huku mtaani unadhani mchina akija eneo lako na akiuza bidhaa kama unayouza wewe utatoboa?
Mwenzako anaongea kichina na bidhaa zinatoka kwao bei yk anakuja nayo ya chini kabisa sasa huwezi kumzidi kwa chochote.
 
they are more aggressive kuliko sisi, badala ya wewe kushukuru sasa angalau unauzia nyanya zako shambani, unawalaumu wakizuiwa, nyanya zako zitaozea shambani utaanza kulialia!
P
 
Wenzetu wana mitaji mikubwa serikali inawakopesha. Wachina wanapewaga kati ya 200M mpaka 500M per head kuja kuanzisha biashara Africa huku.

Anajipanga kuanzia kiwandani analipa 50% ya fedha anachukua mzigo kwa mali kauli kwa guarantee ya serikali. Wakija huku fursa wanaziona kwa haraka sababu vitu vingi walivyonavyo sisi hatuna.

Niambie ili upewe 200M bongo utahitaji kuzungushwa miaka mingapi?😂 Mikopo tu ya million 10 mtaambiwa mjipange muende kama wanakijiji 🤣 na huo mkopo kupewa mtazungushwa mwaka mzima.
 
they are more aggressive kuliko sisi, badala ya wewe kushukuru sasa angalau unauzia nyanya zako shambani, unawalaumu wakizuiwa, nyanya zako zitaozea shambani utaanza kulialia!
P
Nasema kinachoonekana mkuu. Mimi nifaida kwangu huu ndo ukweli. Lakini tatizo lipo kwenye Nchi yetu maana nyanya zinazo enda Rwanda na Kenya wanenda kusindika Ili Hali hata sisi kama serikali ingeleta wawekezaji wa maanatungeuza Kwa bei ya utupwa. Kipindi Cha himaya nyani mipaka ilifungwa nyanya zikashuka bei sana. Hii yote serikali haimjari mkulima. Ukiangalia hatuna viwanda vya kusindika nyanya zetu zikikoswa wateja siku3 Zina haribika zote!!


Serikali iwekeze kwenye viwanda tusindike na tuuze Nje mkuu. Hapa ni jukwaani Sioni kitu Cha kuficha Hali halisi ndo hii. Ahsantee
 
Sheria za uwekezaji zinasemaje kuhusu raia wa kigeni? Kazi za kimachinga nadhani hawatakiwi kuziingilia, lakini mamlaka husika ziko kimya, wako busy na uchaguzi
Wachina watazidi kumiminika sana bongo sababu mazingira ni rafiki. Bongo sheria ziko imara kwa maskini tu ila ukiwa na hela unahonga maaskari maisha yanaenda. Wao wanapokuja huku wanakuja na hela. We unamuona machinga ila ana hela ya kutosha ndio maana huwezi kukuta mchina anaishi Tandale au Vikindu wengi wamechukua apartments za kodi za laki 5 au zaidi kwa mwezi tena mostly wanaishi prime areas kama Kariakoo, Upanga, Oysterbay na Masaki.
 
Una hoja ,ila sidhani kama anazijua Sheria za uhamiaji.
 
🤣

Wachina wanapewa mikopo na serikali yao. Pia wanapewa mali za mabilioni toka viwandani kwao kwa mali kauli. China viwanda ni vingi kuliko mahitaji na bidhaa ni mafuriko na wana changamoto ya uzalishaji wa bidhaa uliopitiliza, surplus industrial production. Kwa hiyo wakiona nchi yoyote imelegealega wanaifanya soko..



Pia wachina wako bongo kutokana na material za ubora wa chini ambazo ni reject sehemu zote duniani hasa ulaya na Marekani ila kwa nchi za kiafrika zinakubaliwa.



Nakupa siri nyingine kwa nini wachina wako bongo wengi mno. Ni profit margin ya juu ambayo wafanyabiashara wa kitz ambao wanaagiza vitu toka nchini kwao. Profit margin ya watz ukilinganisha bei ya kununua china+usafiri+kodi na bei ya kuuza Tz ni kama mara 2 mpaka mara 15+. Ndio maana wachina wanafurika. Na wanajenga kituo cha biashara zao na viwanda vyao huku Tz Ubungo. Hiyo kariakoo itabaki stori tu 🤣🤣
 
WACHINA siyo wakuwaendekeza, kazi wanazofanya hapa kwao hawakubali tufanye. Sheria ichukue mkondo wake wakabanane huko huko kwao.
Bongo sheria haifanyi kazi kwa mtu mwenye hela. Hao wasimamizi wa sheria ndio wala rushwa wakubwa na wachina kwa kujua hilo ndio wamezidi kuitana nchini.

Sahizi ukienda maeneo ya nyuma ya Kinondoni Morocco Square kule unaweza dhania upo Ghanzhou😄 au Shenzen. Kule ndio wamejitwalia block nzima wamejenga apartments na supermarket zao za kichina na migahawa. Sidhani kama sheria zao zinaweza kuruhusu mbongo akanunue ardhi na kufanya yale yaliofanywa pale Kinondoni.

Ila sababu mamlaka zimeruhusu hayo sisi ni nani hata tupingane na mamlaka. Japo kisheria haliko sawa.
 
Mkienda nchi yao huwa mnaenda kufanya kazi gani?.
Kariakoo sishangai sababu kwenye maduka yao, machinga wameziba hadi milangoni kwao... Mnategemea watafanya nn?. Kuna Wamalawi, Wakenya, Waganda, n.k wanafanya umachinga kkoo na hakuna anayeropoka asa iweje Wachine muwabughudhi?
 
Mimi nina mtu Kinglion pale😂 jamaa wanauza sana mapikipiki mikoani. Hesabu zao wanazofungakwa mwaka its billions za kutisha 🤣. Kodi wanakwepa ile laana na wako njema kwenye kuhonga mamlaka.

Jamaa wanapiga hela sana, mtu anakuja na mtaji kidogo after 5 years ni billionaire wa kutupa. Nadhani baada ya wahindi na warabu hawa jamaa ndio watakuja ku take over kwenye utajiri bongo.
 
Mimi nina mtu Kinglion pale😂 jamaa wanauza sana mapikipiki mikoani. Hesabu zao wanazofungakwa mwaka its billions za kutisha 🤣. Kodi wanakwepa ile laana na wako njema kwenye kuhonga mamlaka.
🤣 watu wengi wanawachukulia poa wachina. Ila hao wachina wanaifanya biashara ya mabilioni ya hela. Mimi kuna jamaa yangu yumo kwenye chain ya vifaa vya ujenzi vya kichina hasa mabati. Jamaa anasema wanafanya biashara za mabilioni. Boss wao Mchina anataka kujenga viwanda nchi nzima kila wilaya 🤣
 
😂 Sio kila mbongo ni mduanzi. Kuna watu smart ila ndo hao weupe wana ubaguzi. Mhindi hana shule anakuja kupewa nafasi ya kiuongozi kwenye kampuni ya muhindi mwenzake. Anatolewa mtu mwenye CPA anawekwa form 4 mwenye cheti cha uhasibu amuongoze mtu mwenye CPA wale jamaa ni mikwunduw sana siwapendi wahindi na kama nikipata urahisi watu wa kwanza kuwafukuza itakuwa wao.

La hashaa wakubali kulipa mishahara mizuri kwa wazawa ambao ni sawa na wanavyolipa wahindi wenzao.
 
Hela wanapata sana, yani mtu anauza unit moja anapata faida 10 folds. Utaachaje kufungua viwanda kila kona. Unaanza na mtaji wa 200M ukimaliza mzigo una billion 2. Utaachaje kufungua viwanda kila kona.🤣

Halafu nachowapendea wachina hawana tabia za kishenzi kama wahindi. Mchina akipiga hela anakuachia gepu na wewe uishi.
 
Hela wanapata sana, yani mtu anauza unit moja anapata faida 10 folds. Utaachaje kufungua viwanda kila kona. Unaanza na mtaji wa 200M ukimaliza mzigo una billion 2. Utaachaje kufungua viwanda kila kona.🤣
Kiufupi hao jamaa wamejipanga kupata utajiri. Ila kuna ubaguzi wa rangi kwenye taasisi Tanzania, mchina akitaka kuanzisha kiwanda anahudumiwa harakaharaka
Akitaka kiwanja (industrial plot)anapewa fasta na hati fasta, vibali anapata fasta, kodi wanapunguziwa fasta, bandarini kilakitu wanafanyiwa fasta,umeme unawekwa kiwandani FASTA,tbs fasta, anazalisha bidhaa fasta zinaingia sokoni fasta. Ukiachana na rushwa pia kuna kama ubaguzi wa rangi kwenye taasisi zinazohusika.



Ukienda wewe ngozi nyeusi utazungushwa mpaka upate kizunguzungu 🤣
 
Wanajua kuitumia mithali hii: Aliyelala usimwamshe!
Watanzania tunalala mno.
Kama kwa ripoti ya sasa hivi inasema 87% ni Tegemezi ina maana(ukiondoa Watoto,Wazee na Walemavu) wavivu ni wengi.
 
Kinachofanya watu wajazane kwenye umachinga ni lack of government support. Hatuna viwanda vingi sasa utaishije bila kazi. Lazma uanze kuuza makava na chaja za simu bila kusahau sumu za kuua mende na kunguni😂 ilimradi mkono uende kinywani.

Ila kungekuwa na large scale productions masoko ya chakula tu yapo nchi nyingi zinazotuzunguka. Tumekuwa na bahati mbaya na serikali ambayo haina vipaumbele vya kubadilisha maisha ya watanzania kwa dhati. Tunakazana na mambo ambayo impact yake ni ndogo kwa social welfare.
 
Hakuna miujiza hapo, ni 10% na wale ndugu zetu hawanaga mkono wa birika wakitaka mambo yao yaende. Mwekezaji anakuja na $30 millions ila katika hizo hela anajua atatumia $3 millions ili kuweka mambo sawa. Wameshaambiwa na wenzao walioko huku kuwa bongo panaingilikaje.

Kama unavyotujua wabongo wakitaka rushwa viswahili huwa ni vingi na kuzungushana. Wao huwa wanadili na mamlaka za juu tu. Kamishna anawekwa kwapani, Mkurugenzi wa TBS kwapani, Waziri wa ardhi kwapani wakimaliza na IGP kwapani biashara imeisha.
 
Wazawa watafanya shughuli gani?


Kwani mnyie mnapoenda nchi za watu huwa mnaenda kufanya shughuli zipi? Huwa mnaenda kuwekeza na kufungua viwanda?

Acheni hizo, waacheni wafanye kile wanachokiweza ili mradi hawavunj sheria. Wakiwafanyieni hivyo kwao mnawaita wabaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…