Dar: Raia wa China wageuka machinga, Wananchi washitushwa

We jidanganye kuwa mchina ni mwenzako. Nionyeshe shule, hospital au miradi ya maji ili jengwa kwa msaada wa WACHINA ili iwasaidie wazawa.
Huwa nashangaa sana, kwahio mtu akiwapa misaada ndio anakuwa mtu wa maana kwenu. Nyie kwanini msijitume kuijenga nchi yenu
 
Nahisi wachina wana mashushushu wa kibiashara Tz. Jamaa wamejipanga kuliko unavyofikiri. Kuna jamaa yangu alihusika kuanzisha kiwanda from A mpaka Z. Jamaa walipata industrial plot na hati fasta. Je ushawahi kusikia industrial plot inauzwa? Ila hao wachina walienda huko Ardhi fasta wakapata eneo. Wakajenga kiwanda fasta wakakimbiza kila kitu FASTA FASTA kiwanda kikaanza kazi. 🤣🤣🤣. Wachina wako vizuri mno 🤣 yaani connection+10% ni balaa
 
Hiko si kielelezo, kuna limit kisheria kwamba kazi zipi zinaruhusiwa kufanywa na wageni ili kulinda kazi za wazawa, huwezi kumruhusu mtu afanye umachinga kisa kapanga apartment ya gharama
Hiyo ni personal life yake

Gov isipodhibiti hilo now, hali itakuwa mbaya mbeleni
 
Nenda china kama hawajakuua? Ni wabaguzi sana wa rangi! Kuna watz wengi sana wameuwawa na walikuwa wanasoma! Washenzi sana Hawa!
 
WaTz uaminifu ni bidhaa adimu, wacha tunyooshwe.
 
binafsi sioni shida yeyote mchina akiuza hata chips.

Mgeni yeyote anapoingia nchi yeyote kufanya chochote lazima apewe vibali na mamlaka za nchi husika kufanya hicho anachotakiwa kufanya.

Nenda china leo hii kaombe kibali cha kufanya biashara ya umachinga mitaani.
 
Nchi imefunguliwa,
Wachina ni ndugu zetu, mabeberu ni mashoga😁
 
Naona kama wanalinda mizigo yao baada ya kuibiwa kupitiliza na wezi wa kko!
 
Yaani hapo eti mtu mwenye mamlaka ndiyo ameagiza! 🤣🤣🤣🤣🤣
 
Nchi yetu hivi sasa inapita kwenye majaribu makubwa,mtu anaweza akatoka kokote akaja kuchezea Watanzania kadri awezavyo.
 
Hivi idadi ya wachina nchini ikifika robo ya idadi ya watanzania kiuchumi nchi itakuwaje?

Pia nashauri mamlaka izibe mianya ya wachina kutorosha pesa nje. Wanachokipata waendelee kukiwekeza hapa hapa kwenye kujenga viwanda n.k. Hope miaka 10 ijayo Tanzania tutakuwa wazalishaji wakubwa kwenye viwanda.
 
Wachina watageuza Tz kuwa jalala la kutupia bidhaa zao zinazokataliwa ulaya na Marekani
 
Wazawa wanataka wawe wamachinga wageni ndio wamiliki viwanda 😆
 
“Kama biashara haifai kufanywa na watu wa nje wasifanye, sababu ni nini mpaka wanapewa leseni ya kufanyabiashara za aina ile, na kama hawapewi leseni kwanini wanafanyabiashara za aina ile.”
Babu wa Babu zao walijenga reli ya kati walifia kwenye miamba, makaburi yao yapo mpaka kesho hapo kambi ya Jeshi ukonga Gongo la Mboto km unaelekea Pugu kushoto kwa hio Mimi siwachukulii km Wageni watu km hao nawachukulia km ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…