Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Dar: Sakata la Polisi kuuana wenyewe nje ya benki laacha sintofahamu

Jeshi la polisi limeharibika lote linahitaji intesive reformation ili liwe zuri nadhan ndo jeshi la polisi bovu ukanda afrika ukitoa msumbiji kwa sasa
 
duuu, hapo ndo ujue kuwa weled ktk jeshi letu la polisi hamna kabisa, pia ata mwanajeshi hakuwa na hekima hata kidogo na anatakiwa kuadhibiwa vikali, haiwezekan umeshapewa tahadhali ya kutoka eneo hilo na unaona kabisa kitu kinachoendelea kwa mjibu wa sheria na kiusalama, halafu ww unadinda eti kisa ww ni mwanajeshi yaan alishindwa kutambua kwamba hapo kuna tukio linalohitaji usalama zaid, na alikosea zaid alipoishika silaha ya afande kama ni kweli, hapa polisi walitakiwa wamkamate kwa nguvu then wampe kichapo cha mbwamwitu ili ajue kuwa kaingia cha kike, askali aliyerusha risasi hakutumia weled wa kazi.
Hapo unaposema alikosea zaidi kushika silaha ya askari, soma vizuri mada utaelewa kwanini alifanya hivyo.
 
Awamu hii kila mtu mwenye kanafasi anajiona mkubwa kuliko mwingine.

Hapo navyojua wajeda lazima walipe kisasi kwa mwenzao kudharauliwa.

Huyo FFU aliyefyatua risasi sidhani kama ana amani kwa sasa.
Duu sio kwa hiyo kichwa yako nani atalipwa kisasi na hiyo amri itatolewa na kiongozi yupi wa jw
 
Acha wafu wazike wafu wao sio police imekua kawaida kutumia bunduki kuua raia kwa hiyo amna jipya
 
Daaaah pole sana mwanajeshi na sijui kwanini hakumnyanganya kabisa ile bunduki na kulenga yule pimbi aliyekuwa amebaki kwenye gari nawachukia sana hawa mbwa wa kaki ***** zao narudia tena pole sana mwanajeshi Mungu akufanyie wepesi upone haraka
dah polisi ni hawa hawa ndungu na marafiki zetu tunaoishi nao mitaani.
 
Pole mjeshi. tatizo nchi hii wanajeshi tunawachezea kama shemeji zetu, nadhani ametoa somo. wanajeshi waheshimiwe! wasichokozwe bila sababu. matokeo ya askari hata kulenga shabaha hajui! Wanajeshi wapewe heshima yao, wao hawakurupuki ktk mamuzi yao. nadhani alidharauliwa sana mpaka kuingia kwenye ugomvi huo. Upone haraka mjeshi urudi kulitumika taifa letu pendwa🙁
huyo mwanajeshi atashtakiwa kwa mauaji
 
UWAZI LAMRUDIA MAMBOSASA
Uwazi lilimrudia tena Kamanda Mambosasa na kumtaka kulizungumzia tukio hilo ambapo alikiri na kusema kuwa, kulikuwa askari waliofanya tukio hilo walimdhania mwanajeshi huyo kuwa ni jambazi.

Mkuu kabisa kanda maalum anaongea hiyo kauli,,, hivi unawezaje kudhani ni jambazi? kwa ishara gani aliyoionesha huyo mwanajeshi?
Kakataa amri na kuishika silaa ya askari
 
mengi yameandikwa, sijaona benk ikitajwa. utaratibu wa benk kuweka pesa atm una dosari. wateja wangeelekezwa na benk kuondoka na si police, ambao wa ngazi za chini pr yao ni 0-ve.
 
Wangekuwa wanauana wenyewe kwa wenyewe wala isingekuwa shida!
 
Niwashauri chuo cha polisi au jeshi?! Aliyetakiwa kuwa na nidhamu na utambuzi hapo ni nani kati ya polisi na mwanajeshi?
Mwanajeshi amewatambua polisi na ndio maana hakua na wasiwasi kwakua alijiona yeye ni mwenzao (kuna msemo unasema meno ya umbwa hayaumani).. sasa inaonekana polisi walishindwa somo la utambuzi kwa mwanajeshi, nidhamu (kwa maana ya kutuliza temper) na silaha (wakati gani sahihi kuitumia).

mleta madaanakwambia mwanajeshi aliongea kiistaarabu na alihiitaji angeambiwa aondoke kistaarabu pia.

ukweli usiopingika, hawa vijana wadogo wadogo wa sirro wa intake za hivi karibuni hawana mafunzo mazuri.

ukiendelea kubisha utakua umedhamiria kubishana na sio kuelewa.
 
Huyu mwanajeshi ni hodari wa kujikinga.
Nahisi aliona mfyatua risasi anamlenga kisha akamuweka polisi kama kinga.
Polisi haruhusiwi kufyatua risasi kwa mtu ambaye hana silaha.
Ingetokea mwanajeshi amemnyang'anya polisi silaha na kutaka kuitumia kupiga, polisi angekuwa na haki ya
kutumia silaha yake.
Kuna mapungufu makubwa sana kwa polisi wetu katika kanuni za kutumia silaha za moto wakati wa matukio madogo.
Kaa kimya usichokijua kuhusu silaha
 
maelekezo ya kipuuzi na ya kibabe ndio chanzo cha yote haya.walioendelea wanatenda kama hii mipuuzi yetu ? sio wote namaanisha baadhi ya mipuuzi yetu !!
Tofautisha wakati wa kutumia command na polite language acha ujuaji kwa kitu usichokijua
 
Vyuma vyuma dadekii.. Watu wana frustrations vibaya.
 
Ninachowaza ni huyu polisi alikuwa kamnyooshea huyo mwanajeshi bunduki kutokea umbali gani, ukiangalia vizuri mwenye tatizo ni huyu polisi maana itakuwa alienda msukuma mjeshi kwa kutumia bunduki labda ndio sababu ya mjeshi kuamua ishika kuielekezea juu

Anyway niishie hapo
 
Tatizo watanzania wengi ni ushabiki na hatujui usafirishaji wa pesa unakuawaje au sheria zake zipoje? Na kutofautisha kauli na mahali kuna kipindi lazima voice of command itumike na kuna kipindi au mahala unapaswa kutumia polite language

Tuache ushabiki wa kipimbi huyo mtu alie taka kumpora askar bunduki mnajua alikuwa na nia gani? Bunduki haimui askar tu hata wew na watu wengne itawaua tu sheria lazima izingatiwe

Hata wew ukiwa eneo lako la kazi lazima utumie command pale unapoona mtu anakudharau tuache unafki
 
Back
Top Bottom