Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye

Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye

Hawezi kuendesha huduma muda wote huo bila kibali, ni vita ya kiuchumi tu hapo.

Mimi siyo muumini wa hizi NGO lakini natowa ushuhuda kuna Dada namjuwa fika alipata upofu kwa miaka kadhaa na ninaamini ulikuwa ni ushirikina, alimaliza hospitali zote, na alimaliza makanisa yote lakini alipata uponyaji kwa Suguye na Sasa anaona kama kama zamani.

Naweza kulishuhudia hili pasipo na shaka yoyote, ingawa Mimi binafsi sina imani na watu hawa.

Siku ukiwajua hao nanabii na miujiza yao utashangaa San. Unatupiwa kitu wanakitoa wenyewe.
 
Mfano wa Kagame, anaetaka kuanzisha kanisa ni lazima awe na degree ya Theology kutoka chuo kinachotambulika na serikali. Nami niongezee, awe na degree ya falsafa kutoka chuo kinachojulikana.
Injili haiendi hivyo.Mungu haitaji chuo,umuinua yeyeto amtakae.
Kagame ni mpita njia hatoishi milele, lakini dini uishi milele
 
Huduma za kiroho katika Kanisa la The
Word of Reconciliation Ministries (WRM) la Kivule- Matembele ya pili, jijini Dar es Salaam zimesitishwa huku ulinzi wa Jeshi la Polisi ukiimarishwa ili kuzuia huduma yoyote isifanyike.

Huduma ya kanisa hilo lililo chini ya Nabii Nicolaus Suguye imezuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita, huku waumini zaidi ya 4,000 wakidai kupewa maelekezo ya kutakiwa
kutafuta maeneo mengine ya kuabudu.

Vyanzo vinaeleza kanisa hilo lilikuwa ni miongoni mwa taasisi ambazo hazijapata usajili rasmi, isipokuwa barua ya usajili wa awali inayoruhusu kufanya huduma sehemu moja bila kualika
wageni kutoka nje, kufungua matawi na kufanya
makongamano huku Serikali ikifanya uchunguzi wa mwenendo wake.

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema kwa sasa anayelalamikia si yeye (Suguye) kwani yeye anajua kanisa halina usajili na anajua
kwa nini amefungiwa.

Mwananchi tangu juzi na jana iliwatafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni na naibu wake, Jumanne Sagini ambao taasisi za dini ziko chini ya wizara yao, lakini hawakupokea simu na wakati mwingine zilizimwa.

Msemaji wa wizara hiyo, Christina Mwangosi alipokea simu mara moja na alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo aliomba apigiwe baadaye.
Hata hivyo, alipotafutwa baadaye hakupokea tena na mwandishi alipofika ofisi za msajili wa taasisi hizo jijini Dar es Salaam alikutana na maofisa waliomwambia hawawezi kulizungumzia suala hilo isipokuwa msemaji.

Suguye, anayetambuliwa na waumini wake kama nabii, alianza kutoa huduma za kiroho mwaka 1998 kabla ya kuanzisha kanisa hilo mwaka 2007.
Hapa kuna hujuma za kiroho na siyo huduma. Hawa ni matapeli na wavivu wa kutafuta wanaowatia wajinga na wapumbavu wetu wengi waliokata tamaa ujinga na umaskini. Heri lingebomolewa akauze nyanya.
 
Bado mzee wa upako.yaani saa hivi ni mwendo wa kuwasambarisha matapeli walijificha nyuma ya dini huko kuna maharamia kibao wa nchi jirani wanajifanya walikole/wachungaji
 
Tuwe wabia mkuu,
natoa eneo, na nakua mweka hazina wa kanisa
wewe uwe mtumishi.

Karibu sana tutafute watu wa kuigiza wana mapepo kama watano tu af sisi tukafungue kigamboni kule au ilala
 
cha kushangaza wanajifanya welevu sana, kumbe ni matahira

Shemeji yangu humuambi kitu kuhus Mwamposa kipindi yupo mjamzito alikuwa anaenda kila siku asubuhi alikuwa anasema kuna clinic yao huko kwa Mwamposa
 
Back
Top Bottom