MLEVi Mmoja
JF-Expert Member
- Jun 29, 2019
- 8,514
- 15,050
Hivi wizara ya afya na mental problems jumlisha wizara ya mazingira wao wanajua kuandikiana posho na visemina vya hapa na pale ili tu wapate perdiem Ila kuwalinda watu a mabosi wao tuliowapatia kazi hawajui kabisa wamejisahau kwa kulewaa madaraka tuliyowapatiaMimi hapa kuna jiran ana sherehe kapig mziki mpak saa sita nimemfwata nimemuambia tunatak kulala amepunguza sasa
Hivi wizara ya afya na mental problems jumlisha wizara ya mazingira wao wanajua kuandikiana posho na visemina vya hapa na pale ili tu wapate perdiem Ila kuwalinda watu a mabosi wao tuliowapatia kazi hawajui kabisa wamejisahau kwa kulewaa madaraka tuliyowapatia
Hopeless point.Kanisa katoliki wanauza rozali, wanauza vitabu na hadi bar za kuuza pombe wanamiliki, anayebisha aende Msimbazi center na maporokia mengine hukosi bar ya kuuza pombe.
Nami nasisitiza wapitiwe wote hao mwamposa,musa,sila mtui na wengine wanapiga hela ambazo hatahawalipi kodi wanakusanya mahela kwa usanii tu.Hellow
Serikali imeingilia kati huduma za kiroho zitolewazo kanisa la WRM kivule maarufu kwa nabii Suguye mpaka sasa hawajatoa sababu maalumu ya kuzuia huduma hizo kusitishwa kwenye kanisa hilo.
Kwa upande wangu kama walivyo chunguza hilo kanisa na kugundua mapungufu yaliyopo basi wafanye hivyo kwa Mwamposa pia japo watu wanaosali huko kwa Mwamposa wakisikia unamponda watakujia juu as if walizaliwa huko.
Na baada ya hapo pia mchunguzeni pia Kuhani Musa nae ana jambo lake yule msihishie hapo tu piteni, na kwa Gwajima hawa watu wana kula hela za masikini acha leo tuwapazie sauti wanyonge hawa labda watatukumbuka huko mbeleni.
Mkalitazame na mnipe mrejesho nawasilisha.
========
Huduma za kiroho katika Kanisa la The Word of Reconciliation Ministries (WRM) la Kivule- Matembele ya pili, jijini Dar es Salaam zimesitishwa huku ulinzi wa Jeshi la Polisi ukiimarishwa ili kuzuia huduma yoyote isifanyike.
Huduma ya kanisa hilo lililo chini ya Nabii Nicolaus Suguye imezuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita, huku waumini zaidi ya 4,000 wakidai kupewa maelekezo ya kutakiwa kutafuta maeneo mengine ya kuabudu.
Vyanzo vinaeleza kanisa hilo lilikuwa ni miongoni mwa taasisi ambazo hazijapata usajili rasmi, isipokuwa barua ya usajili wa awali inayoruhusu kufanya huduma sehemu moja bila kualika wageni kutoka nje, kufungua matawi na kufanya makongamano huku Serikali ikifanya uchunguzi wa mwenendo wake.
“Baada ya uchunguzi wa mamlaka za usajili imeonekana huduma ya WRM imepungukiwa sifa za kupata usajili kamili, hivyo ikapewa notice ya kuzuiwa kuendelea na shughuli, ikisajiliwa ataruhusiwa kuendelea na shughuli za kutoa huduma ya neno la Mungu,” kilieleza chanzo.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema kwa sasa anayelalamikia si yeye (Suguye) kwani yeye anajua kanisa halina usajili na anajua kwa nini amefungiwa.
Muliro alisema wao ni wasimamizi wa sheria na wanapaswa kuzilinda, “na kama (kufungiwa) ingekuwa ni kinyume cha sheria au taratibu unafikiri wenye kanisa wangekaa kimya? Kuna vitu haviko sawa kuhusiana na taasisi hiyo ya dini na lazima vitimie.”
Suguye, anayetambuliwa na waumini wake kama nabii, alianza kutoa huduma za kiroho mwaka 1998 kabla ya kuanzisha kanisa hilo mwaka 2007.
Kanisa hilo limefungwa ikiwa ni mwaka mmoja baada ya wizara hiyo chini ya ofisi ya Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa kutangaza mabadiliko ya hadhi ya vyeti vya usajili wa taasisi za kidini na jumuiya mbalimbali za kijamii inayoelekeza kuhuisha vyeti vya usajili kila baada ya miaka mitano.
Pia limefungiwa ikiwa ni miezi minne baada ya Nabii Suguye kuibua mjadala ufunuo wa kucha na nywele, akidai Mungu wake kuagiza waumini kutoa kucha za kidole cha mwisho cha kushoto (mguu na mkono) na nywele za utosini na paji la uso kisha kufunga kwenye kitambaa cheupe ili awaponye.
Kisheria ili kusajili taasisi hizo za kidini, mwombaji anatakiwa kuwa na nakala za katiba, kujaza fomu mbili yenye wasifu wa viongozi, muhtasari wa vikao, kulipia ada ya maombi ya usajili, ada ya usajili, ada na tozo ya kila mwaka baada ya kusajiliwa na kuwasilisha ripoti ya utendaji na fedha ya kila mwaka.
Si Sadaka tu,kumuona ofisini kwake hadi utoe laki mbili +.Mmoja wa manabii wa uongo, mission town, tapeli, anayechukua sadaka za watu kwa kutumia jina la Yesu Kristo.
Wasiishie kufunga hilo yako mengi sana ambayo ni kero kwenye jamii
Nami nasisitiza wapitiwe wote hao mwamposa,musa,sila mtui na wengine wanapiga hela ambazo hatahawalipi kodi wanakusanya mahela kwa usanii tu.
Pia limefungiwa ikiwa ni miezi minne baada ya Nabii Suguye kuibua mjadala ufunuo wa kucha na nywele, akidai Mungu wake kuagiza waumini kutoa kucha za kidole cha mwisho cha kushoto (mguu na mkono) na nywele za utosini na paji la uso kisha kufunga kwenye kitambaa cheupe ili awaponye.
Katika ukristo kuna Roman catholic,,Protestant yenye madhehebu yaliojiengua roma e.g kkkt,moravian na anglican,,,na upande wa pili wa protestant kuna Pentecoste church e.g FPCT,TAG,,PAG nk nk na part ya mwisho ni JW,,mormon na Watakatifu wa siku za mwisho. Kwa hio wa mafuta chumvi na maji anaweza kuwa regulated na kuwa filtered na Pentecostal Church na hao Pentecostal church wanaweza kushirikiana na madhehebu mengine wakaja na utaratibu mmoja ulio rasmi.Kwa sababu kinachofanya makanisa yanakuwa mengi na mengine yenye walakini ni kukosa filter na utaratibu.Sasa hata wewe unaweza ukasuggest utaratibu uweje.Imani si suala la ujumla mpaka ulazimishe watu wa Makanisa fulani wasimamie wenzao wakati imani zao haziendani.
Ndo maana Serikali yenyewe INASAJILI Makanisa na Madhehebu kwa vigezo vyake, huwezi kuwapa Makanisa fulani nguvu juu ya wengine huku tukisema kuwa Serikali yetu haina DINI wala DHEHEBU.
Leo hii kuna waoamini kwenye Mafuta, Maji, Vitambaa, Zabibu... Wengine imani yao hairuhusu kudungwa sindano hata kama wanakiona kifo.. Sasa kwa huu mvurugano yupi utampa MAMLAKA juu ya wengine.
Udini haujifichi ni kama giza na mwangaHili swali lipo VALID kwa muda wote..!!
By the way, pengine sasa ndo kakiuka masherti ya usajili
Wewe sio mkristo ni mpembaHakuna udini hapo Acha kujipaka damu..Sisi wakristo tunaojielewa hatuwezi kuona udini
Hata Mungu hana demokrasia maana yeye ni mfalme,,,demokrasia ndio imeshaprove failure kwenye kusajili makanisa.Katika waisraeli maelfu kwa mamia waliotoka misri ni wawili tu waliofika kaanani japo hao waliofia njiani watoto wao ndio walioingia nchi ya ahadi...Na hata kuingia mbinguni kuna mchujo tena mkali wachungaji,,mitume ,,mapadre na makasisi wengi sana watafeli na hawataingia mbinguni..Na hizi nchi za weusi kama mimi usitegemee demokrasia kutuletea matokeo chanya..Mawazo ya kidikteta, hakuna mtu au taasisi yenye hatimiliki na dini. Nani kakuambia TEC au umoja wa makanisa ya kipentekoste ndio n.k ndio vipimo sahihi vya dini ya Kikristo ?
Ndiyo Nabii Mkuu PaleSuguye ndiyo nani?
Wacha uzushi na fitna weweUdini awamu ya sita inatisha sana
Umeeleza vizuri kabisa Makanisa yetu yalivyo,,, but swala la imani litabaki kuwa la mtu binafsi unless kuna madhara ya wazi ya kiafya ndani au nje ya mwili pengine ndiyo vyombo vya Serikali viingilie, mfano yule jamaa wa SA aliyekuwa analisha waumini wake PANYA wazima..Katika ukristo kuna Roman catholic,,Protestant yenye madhehebu yaliojiengua roma e.g kkkt,moravian na anglican,,,na upande wa pili wa protestant kuna Pentecoste church e.g FPCT,TAG,,PAG nk nk na part ya mwisho ni JW,,mormon na Watakatifu wa siku za mwisho. Kwa hio wa mafuta chumvi na maji anaweza kuwa regulated na kuwa filtered na Pentecostal Church na hao Pentecostal church wanaweza kushirikiana na madhehebu mengine wakaja na utaratibu mmoja ulio rasmi.Kwa sababu kinachofanya makanisa yanakuwa mengi na mengine yenye walakini ni kukosa filter na utaratibu.Sasa hata wewe unaweza ukasuggest utaratibu uweje.