Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye

Dar: Serikali yalifunga Kanisa la Nabii Suguye

Mimi hapa kuna jiran ana sherehe kapig mziki mpak saa sita nimemfwata nimemuambia tunatak kulala amepunguza sasa
Hivi wizara ya afya na mental problems jumlisha wizara ya mazingira wao wanajua kuandikiana posho na visemina vya hapa na pale ili tu wapate perdiem Ila kuwalinda watu a mabosi wao tuliowapatia kazi hawajui kabisa wamejisahau kwa kulewaa madaraka tuliyowapatia
 
Mimi nashindwa kuelewa kuna watu kutoka Nigeria na DRC wanakuja kufungua makanisa hapa nchini, serikali ipo kimya tu. Hii nchi kila mgeni anakuja anavuna anaondoka. Kuna makanisa ya mbavu za mbwa huko Kivule na Ukonga yanasimamiwa na kuendeshwa na Wakongo.
 
Hivi wizara ya afya na mental problems jumlisha wizara ya mazingira wao wanajua kuandikiana posho na visemina vya hapa na pale ili tu wapate perdiem Ila kuwalinda watu a mabosi wao tuliowapatia kazi hawajui kabisa wamejisahau kwa kulewaa madaraka tuliyowapatia

[emoji23][emoji23][emoji23] wapo bize kutembea mikoani
 
Hellow

Serikali imeingilia kati huduma za kiroho zitolewazo kanisa la WRM kivule maarufu kwa nabii Suguye mpaka sasa hawajatoa sababu maalumu ya kuzuia huduma hizo kusitishwa kwenye kanisa hilo.

Kwa upande wangu kama walivyo chunguza hilo kanisa na kugundua mapungufu yaliyopo basi wafanye hivyo kwa Mwamposa pia japo watu wanaosali huko kwa Mwamposa wakisikia unamponda watakujia juu as if walizaliwa huko.

Na baada ya hapo pia mchunguzeni pia Kuhani Musa nae ana jambo lake yule msihishie hapo tu piteni, na kwa Gwajima hawa watu wana kula hela za masikini acha leo tuwapazie sauti wanyonge hawa labda watatukumbuka huko mbeleni.

Mkalitazame na mnipe mrejesho nawasilisha.

========

Huduma za kiroho katika Kanisa la The Word of Reconciliation Ministries (WRM) la Kivule- Matembele ya pili, jijini Dar es Salaam zimesitishwa huku ulinzi wa Jeshi la Polisi ukiimarishwa ili kuzuia huduma yoyote isifanyike.

Huduma ya kanisa hilo lililo chini ya Nabii Nicolaus Suguye imezuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita, huku waumini zaidi ya 4,000 wakidai kupewa maelekezo ya kutakiwa kutafuta maeneo mengine ya kuabudu.

Vyanzo vinaeleza kanisa hilo lilikuwa ni miongoni mwa taasisi ambazo hazijapata usajili rasmi, isipokuwa barua ya usajili wa awali inayoruhusu kufanya huduma sehemu moja bila kualika wageni kutoka nje, kufungua matawi na kufanya makongamano huku Serikali ikifanya uchunguzi wa mwenendo wake.

“Baada ya uchunguzi wa mamlaka za usajili imeonekana huduma ya WRM imepungukiwa sifa za kupata usajili kamili, hivyo ikapewa notice ya kuzuiwa kuendelea na shughuli, ikisajiliwa ataruhusiwa kuendelea na shughuli za kutoa huduma ya neno la Mungu,” kilieleza chanzo.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema kwa sasa anayelalamikia si yeye (Suguye) kwani yeye anajua kanisa halina usajili na anajua kwa nini amefungiwa.

Muliro alisema wao ni wasimamizi wa sheria na wanapaswa kuzilinda, “na kama (kufungiwa) ingekuwa ni kinyume cha sheria au taratibu unafikiri wenye kanisa wangekaa kimya? Kuna vitu haviko sawa kuhusiana na taasisi hiyo ya dini na lazima vitimie.”

Suguye, anayetambuliwa na waumini wake kama nabii, alianza kutoa huduma za kiroho mwaka 1998 kabla ya kuanzisha kanisa hilo mwaka 2007.
Kanisa hilo limefungwa ikiwa ni mwaka mmoja baada ya wizara hiyo chini ya ofisi ya Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa kutangaza mabadiliko ya hadhi ya vyeti vya usajili wa taasisi za kidini na jumuiya mbalimbali za kijamii inayoelekeza kuhuisha vyeti vya usajili kila baada ya miaka mitano.

Pia limefungiwa ikiwa ni miezi minne baada ya Nabii Suguye kuibua mjadala ufunuo wa kucha na nywele, akidai Mungu wake kuagiza waumini kutoa kucha za kidole cha mwisho cha kushoto (mguu na mkono) na nywele za utosini na paji la uso kisha kufunga kwenye kitambaa cheupe ili awaponye.

Kisheria ili kusajili taasisi hizo za kidini, mwombaji anatakiwa kuwa na nakala za katiba, kujaza fomu mbili yenye wasifu wa viongozi, muhtasari wa vikao, kulipia ada ya maombi ya usajili, ada ya usajili, ada na tozo ya kila mwaka baada ya kusajiliwa na kuwasilisha ripoti ya utendaji na fedha ya kila mwaka.
Nami nasisitiza wapitiwe wote hao mwamposa,musa,sila mtui na wengine wanapiga hela ambazo hatahawalipi kodi wanakusanya mahela kwa usanii tu.
 
Nami nasisitiza wapitiwe wote hao mwamposa,musa,sila mtui na wengine wanapiga hela ambazo hatahawalipi kodi wanakusanya mahela kwa usanii tu.

Hapo utakuta wezake wamemchomesha kati yao hili wachukue wafuasi wake
 
Pia limefungiwa ikiwa ni miezi minne baada ya Nabii Suguye kuibua mjadala ufunuo wa kucha na nywele, akidai Mungu wake kuagiza waumini kutoa kucha za kidole cha mwisho cha kushoto (mguu na mkono) na nywele za utosini na paji la uso kisha kufunga kwenye kitambaa cheupe ili awaponye.

Huo ni ushirikina wa wazi wazi.
Wasirikina wameanza kujidai wanahubiri Neno kumbe wametumwa na Ibilisi ili wapate wafuasi wengi.
 
Imani si suala la ujumla mpaka ulazimishe watu wa Makanisa fulani wasimamie wenzao wakati imani zao haziendani.

Ndo maana Serikali yenyewe INASAJILI Makanisa na Madhehebu kwa vigezo vyake, huwezi kuwapa Makanisa fulani nguvu juu ya wengine huku tukisema kuwa Serikali yetu haina DINI wala DHEHEBU.

Leo hii kuna waoamini kwenye Mafuta, Maji, Vitambaa, Zabibu... Wengine imani yao hairuhusu kudungwa sindano hata kama wanakiona kifo.. Sasa kwa huu mvurugano yupi utampa MAMLAKA juu ya wengine.
Katika ukristo kuna Roman catholic,,Protestant yenye madhehebu yaliojiengua roma e.g kkkt,moravian na anglican,,,na upande wa pili wa protestant kuna Pentecoste church e.g FPCT,TAG,,PAG nk nk na part ya mwisho ni JW,,mormon na Watakatifu wa siku za mwisho. Kwa hio wa mafuta chumvi na maji anaweza kuwa regulated na kuwa filtered na Pentecostal Church na hao Pentecostal church wanaweza kushirikiana na madhehebu mengine wakaja na utaratibu mmoja ulio rasmi.Kwa sababu kinachofanya makanisa yanakuwa mengi na mengine yenye walakini ni kukosa filter na utaratibu.Sasa hata wewe unaweza ukasuggest utaratibu uweje.
 
Mawazo ya kidikteta, hakuna mtu au taasisi yenye hatimiliki na dini. Nani kakuambia TEC au umoja wa makanisa ya kipentekoste ndio n.k ndio vipimo sahihi vya dini ya Kikristo ?
Hata Mungu hana demokrasia maana yeye ni mfalme,,,demokrasia ndio imeshaprove failure kwenye kusajili makanisa.Katika waisraeli maelfu kwa mamia waliotoka misri ni wawili tu waliofika kaanani japo hao waliofia njiani watoto wao ndio walioingia nchi ya ahadi...Na hata kuingia mbinguni kuna mchujo tena mkali wachungaji,,mitume ,,mapadre na makasisi wengi sana watafeli na hawataingia mbinguni..Na hizi nchi za weusi kama mimi usitegemee demokrasia kutuletea matokeo chanya..
 
Katika ukristo kuna Roman catholic,,Protestant yenye madhehebu yaliojiengua roma e.g kkkt,moravian na anglican,,,na upande wa pili wa protestant kuna Pentecoste church e.g FPCT,TAG,,PAG nk nk na part ya mwisho ni JW,,mormon na Watakatifu wa siku za mwisho. Kwa hio wa mafuta chumvi na maji anaweza kuwa regulated na kuwa filtered na Pentecostal Church na hao Pentecostal church wanaweza kushirikiana na madhehebu mengine wakaja na utaratibu mmoja ulio rasmi.Kwa sababu kinachofanya makanisa yanakuwa mengi na mengine yenye walakini ni kukosa filter na utaratibu.Sasa hata wewe unaweza ukasuggest utaratibu uweje.
Umeeleza vizuri kabisa Makanisa yetu yalivyo,,, but swala la imani litabaki kuwa la mtu binafsi unless kuna madhara ya wazi ya kiafya ndani au nje ya mwili pengine ndiyo vyombo vya Serikali viingilie, mfano yule jamaa wa SA aliyekuwa analisha waumini wake PANYA wazima..

Au mfano mtu na akili yake timamu kabisa anakubali kucharazwa fimbo na nabii.... au Binti/Mwanamke anapigwa busu la upako au anaogeshwa na anakubali, sasa hapo utamlaumu nani?
Kwake yeye ni tendo la Imani na huwezi kumkatalia maana ndo maono aliyopewa 😆😆

Kwasababu hata hao SDA, MOROVIAN, KKKT, CATHOLIC, JW, TAG, KPLT, FPCT na mengine yalianzishwa kwa maono ya watu binafsi..

BADO NASEMA IMANI NI SWALA LA MTU BINAFSI, HUWEZI KUKATAA MAONO YA MWINGINE MAANA HATA NA WEWE YAKO HAKUNA MWENYE USHAHIDI NAYO.
 
Back
Top Bottom