DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

DAR: Sheikh wa Mkoa, Mussa Alhad atangaza mwisho wa Mange Kimambi kutukana, kushughulika na JamiiForums kisheria

kwa tafsiri ya vile sheikh alisema, ni Kama shekh ndo mshindi, kwasababu alisema atahakikisha hatatukana tena na ukiangalia ni kweli kwamba mange ameacha kabisa kushambulia watu Kama zamani
Huyu ni sheikh uchwara tu alimuombea mwenzie mabaya na kaumbuka

Uchwara: "...sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake."

Sasa maangamizi gani kayapata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pengo = Alhad sulum

Hawa watu hawana tofauti kabisaaa

Ukitaka kuwaona wewe pambana na ccm ..... Daaa hawana aibu wanavoipigania ccm
 
Huyu sheikh ni matak.o sana na vile anatoa matak.o ndio maana dua yake mbaya kwa Mange imegeuka neema kwa Mange amepata danga la kizungu tajiri ameshanunuliwa gari
 


Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.

=====

Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.

Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.

Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).

Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.


Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.

Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.

Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.

Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi

Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, walijiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.

Na kweli Mange ameacha kutukana
 
Watu wana akili fupi mno humu,shehe hakusema mange atakufa,alisema mwaka huu ndo mwisho wa kutukana,swali mange anatukana au ameacha kutukana?
 
Watu wana akili fupi mno humu,shehe hakusema mange atakufa,alisema mwaka huu ndo mwisho wa kutukana,swali mange anatukana au ameacha kutukana?

Huwezi mtetea shekhe!

Askofu Pengo

Shekhe Alhad

Ni viongozi maarufu wakisiasa kwenye miambali ya makanisa na misikiti respectively

Huwezi kuwasikia wakipambana na matendo maovu ya ccm. Wao hupambana navitu vyakijingajinga Taifa likiangamizwa na ccm

Hawa watu Wa hovyo kwa kuwa na msimamo ya hovyo.

Mange ninani hata ajishrbeduwe kupambana naye? Same tu pengo kila uchao hutoa matamko yakijingajinga tu.
 
Back
Top Bottom