Yamakagashi
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 8,614
- 17,626
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😂😂😂
Kwani Mange umeona siku hizi anatukana?, Amebaki kuuza sura tu huko Instagram hana ishu tena
Mbona aliisha acha kutukana muda mrefu sana sasa. Naona hasira zake ziliisha na aliongeza umri akaanza kujitambua.Na iwe hivyo kama alivyo nena walahi
wamsamehe bure ameshaanza kuunga mkono juhudi za mtukufu kwa haya haya.Kwani Mange umeona siku hizi anatukana?, Amebaki kuuza sura tu huko Instagram hana ishu tena
kwa tafsiri ya vile sheikh alisema, ni Kama shekh ndo mshindi, kwasababu alisema atahakikisha hatatukana tena na ukiangalia ni kweli kwamba mange ameacha kabisa kushambulia watu Kama zamani
Huyo shehe nilikuwa namuheshimu sana lakini sasa hivi nimemdharau kupita bashite
Huyu ni sheikh uchwara tu alimuombea mwenzie mabaya na kaumbukakwa tafsiri ya vile sheikh alisema, ni Kama shekh ndo mshindi, kwasababu alisema atahakikisha hatatukana tena na ukiangalia ni kweli kwamba mange ameacha kabisa kushambulia watu Kama zamani
Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhad Mussa Salim hivi sasa anazungumza na waandishi wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhusishwa na kampeni zinazoendelea katika Jimbo la Kinondoni.
=====
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Mussa Alhad ameelezea picha inayosambaa kwenye mitandao inayomuhusisha yeye kufanya kampeni ambayo yumo yeye na pembeni kuna mgombea wa CCM jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia akila chakula pamoja na wenzake wa CCM. Amesema picha ilipigwa akiwa kwenye maziko ya Sheikh Masoud Ismail, amesema yeye ni kiongozi na mtu yeyote anaweza kupiga picha na yeye.
Amedai Mange Kimambi amekuwa akitukana viongozi mbalimbali kwenye Instagram na kusema pia alimtukana mufti wa Tanzania baada ya kuipongeza serikali na Rais John Magufuli.
Sheikh Alhad amesema ametukanwa kwa dhulma na uadui na kudai Mange anautumia ulimi na mikono yake vibaya kudhulumu watu(Heshima zao).
Alhad amesisitiza huu ni mwaka wa mwisho kwa Mange na baada ya mwaka huu hatamtukana mtu yeyote kwa kutumia ulimi au mkono wake kwa sababu amejihalalishia mwenyewe maangamizi kwa mkono wake. Amesema atamshtaki kwenye mahakama ya Mbinguni.
Amesema kuna watu walimpa rai asimjibu kwani atamtukana sana na kudai wao wanataka aendelee kutukana na hatasikia sauti yake baada ya leo ikimjibu na yeye andelee kutukana.
Alhad amesema hawezi kujiingiza kwenye kampeni ya kuipigia debe CCM, amesema CCM ina kawaida ya kualika viongozi wa dini na chama chochote kinaweza kumualika kwenye jambo lake. Amesema ajabu, picha zake ndio zinaanikwa lakini za viongozi wengine hazianikwi.
Katika hatua nyingine, Sheikh ameiambia NEC kuhusu JamiiForums ambao wameandika kwamba sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam: Hivi mnajua kama anafanya kampeni Kinondoni! Alhad amesema watachukua hatua za kisheria ili wathibitishe sheikh wa mkoa wapi amefanya kampeni, kwa kuhudhuria kwenye maziko au sababu ya picha!.
Juu ya tuhuma za Sheikh kushiriki siasa, soma => Picha za Sheikh Alhad Mussa na makada wa CCM zinatoa tafsiri gani? BAKWATA toeni ufafanuzi
Hivyo kuhusu JamiiForums, wataona namna gani ya kushughulika nao kisheria na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine, walijiingiza katika jambo hilo kichwa kichwa bila kulijua ili kuvunja heshma zao.
Hajaacha kumshambulia Diamond na Zarikwa tafsiri ya vile sheikh alisema, ni Kama shekh ndo mshindi, kwasababu alisema atahakikisha hatatukana tena na ukiangalia ni kweli kwamba mange ameacha kabisa kushambulia watu Kama zamani
Mange kimyaaaaaaWatu wana akili fupi mno humu,shehe hakusema mange atakufa,alisema mwaka huu ndo mwisho wa kutukana,swali mange anatukana au ameacha kutukana?
Watu wana akili fupi mno humu,shehe hakusema mange atakufa,alisema mwaka huu ndo mwisho wa kutukana,swali mange anatukana au ameacha kutukana?