Vijana hawa watano wakazi wa Dar es salaam, TAWFIQ MOHAMED, SEIF SWALA, EDWIN KUNAMBI, HEMED ABASS na RAJABU MDOE wamepotea katika mzingira ya kutatanisha tangu tarehe 26.12.2021 hawajaonekana mpaka leo hii.
Taarifa za ndugu zinasema siku ya mwisho mmoja wao alituma msg kwamba wamekamatwa maeneo ya 'Kariakoo, Kamata' wakiwa kwenye gari IST nyeusi wanapelekwa Central lakini ndugu walipofuatilia polisi Central na vituo vingine vyote DSM hawaonekani. Hata kwenye vyumba vya kuhifadhia maiti miili yao haipo.
Tunaomba kila mwenye kuona asambaze picha hizi au mwenye taarifa apige no hizi.. 0764533335, 0786247106.