Troll JF
Platinum Member
- Feb 6, 2015
- 10,592
- 15,404
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amewakaribisha Watanzania, hususan viongozi wa jumuiya za kiraia, kushiriki mkutano utakaofanyika Mlimani City, Dar es Salaam, kuanzia Oktoba 28 hadi 30, 2026.
Mkutano huo unalenga kujadili changamoto zinazokabili jumuiya za kiraia, kuimarisha ushirikiano na Serikali pamoja na kupendekeza maboresho ya sera, sheria na taratibu zinazohusu utekelezaji wa majukumu yao.
Aidha, washiriki watajadili masuala ya haki, ustawi wa jamii, amani, usalama na mshikamano wa taifa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano huo.
Fika ili uhesabiwe