Dar: Washukiwa wa biashara ya dawa za kulevya watiwa mbaroni

Dar: Washukiwa wa biashara ya dawa za kulevya watiwa mbaroni

Malezi yako mabovu ndiyo yaliyochangia kumharibu mwanao, usisingizie wauzaji wa madawa.
usiseme hivyo ndg.
sio vijana wote wanaoingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya walipata malezi mabovu toka kwa wazazi wao.

miaka kadhaa iliyopita, mtoto wa sheikh mmoja maarufu jijini dar, aliingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya. alilelewa katika misingi na maadili yote muhimu ya kidini na alitimiziwa kila hitaji lake, ila mwisho wa siku akaishia kuwa teja.
 
MAMLAKA ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya jana tarehe 15 April 2020, imefanikiwa kumkamata kigogo wa dawa za kulevya raia wa Nigeria Kanayo David Chukwu (39) mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam.

Pia inawashikilia raia wawili wa Tanzania Alistair Amon Mbele(38) ambaye ni mkutubi wa Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Dar es Salaam, mkazi wa Mbezi Kibanda cha Mkaa na Isso Romward Lupembe (49) ambaye ni mkazi wa Mbezi Louis na Changanyikeni jijini.

Watuhumiwa wamekamatwa na dawa za kulevya aina ya heroin zinazokadiliwa kuwa na zaidi ya kilogramu 270 zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye moja ya nyumba iliyopo Mbezi Kibanda cha Mkaa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo James Kaji amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa muda mrefu nchini na kwamba Mamlaka imefanikiwa kukamatwa kutokana na jitihada ushirikiano uliopo kati ya nchi yetu na nchi nyingine katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya duniani kutokana na utaratibu wa kubadirishana taarifa ambazo husaidia kurahisha ukamataji huo.

“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa vyombo mbalimbali vya usalama ndani na nje ya nchi tulianza kuwafuatilia toka tarehe nane na kufanikiwa kuwaweka mtegoni tangu wakiwa wanateremsha mzigo na kufanikiwa kuwakamata.

"Pia watuhumiwa hao walikuwa wamefanya maandalizi ya kupokea mzigo huo kwa kujenga tenki la maji machafu ambalo liliwekwa chemba juu ya kuhifadhia dawa hizo na bahati mbaya mzigio uliwahi kufika kabla tenki halijakamilika, hivyo kulazimika kuzihhifadhi ndani ya nyumba,"amesema Kamishna Kaji.

Ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na biashara ya dawa za kulevya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania kwa kutoa taarifa pale wanapoona matukio yasiyo ya kawaida kwa usalama.

“Kilo hizi ni nyingi sana zingeingia mtaani zingeathiri nguvu kazi ya vijana wetu huko mitaani kwa kiasi kikubwa. Ninasikitika kuona bado kuna watu wasio na utu wanaendelea kujitafutia kipato kwa njia hii haramu bila kujali. Ninatoa rai kwa watanzania walio tayari kuwapambania watoto wao kuendelea kushirikiana na Mamlaka kuwafichua watu hawa bila woga," amefafanua.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wako mikononi mwa Mamlaka na watafikishwa mahakamani mara baada ya taratibu kukamilika ili sheria ichukue mkondo wake.

View attachment 1420830
Watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya wakiwa chini ya ulinzi baada ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini kuwanasa jijini Dar es Salaam.


View attachment 1420832
Hongera sana Mamlaka. Chapa Kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usiseme hivyo ndg.
sio vijana wote wanaoingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya walipata malezi mabavu toka kwa wazazi wao.

miaka kadhaa iliyopita, mtoto wa sheikh mmoja maarufu jijini dar, aliingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya. alilelewa katika misingi na maadili yote muhimu ya kidini na alitimiziwa kila hitaji lake, ila mwisho wa siku akaishia kuwa teja.
Dini haiwezi kushep tabia ya mtu bali, usimamizi na uwalimu mzuri wa kumuonesha mtoto hadi awe kijana mambo mazuri na mabaya anayotakiwa kuepuka, hebu niambie shekhe ana wake wangapi na wanawatoto wangapi je anakaa na vijana au watoto wake kuwakanya mambo ya hovyo ya dunia?
 
Hongera sanaaaa woote walihusika kukamata hawa wanyama na wauwaji wakubwa
Tuendelee kumuomba mungu atunusuru kwenye hili na pia kwenye corona na mengine ameen
 
Dini haiwezi kushep tabia ya mtu bali.

dini inahusika sana katika ku-shape moral behavior ya mtu. the impact can be positive or negative.

osama bin laden mtoto wa mtu tajiri saudi arabia, katika makuzi yake alipata malezi mazuri sana ya kidini. pia alipata maarifa makubwa ya elimu za kudunia. ila mwisho wa siku akaishia kuwa gaidi aliyetikisa dunia.

usidharau dini.
 
Back
Top Bottom