Dar: Yaliyojiri kuagwa kwa Mwili wa Hayati Dkt. Jonh Magufuli Uwanja wa Uhuru

Dar: Yaliyojiri kuagwa kwa Mwili wa Hayati Dkt. Jonh Magufuli Uwanja wa Uhuru

Wakazi wa Dar wamejitokeza barabarani kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Wakazi wa Dar walionekana kutandika Khanga barabarani ili magari yaliyobeba mwili wa Hayati Magufuli yapite juu yake kuonesha heshima.

Wananchi wengine walikuwa wamebeba mashada ambayo walikuwa wakiyapunga mwili wa Marehemu ukiwa Unapita kuelekea Uwanja wa Uhuru.

Nafuatilia Misa takatifu ya kuuombea mwili wa Aliyekuwa Rais wa JMT, katika kanisa la Mt. Peter kwa hadhi ya msiba ulitakiwa kuwepo na Maaskofu wa kutosha ila sijaona hata mmoja.
Ibada imeendeshwa na Mapadre tu.
Hii si sahihi kabisa.
Rais hakua kiongozi wa kidini.
 
Tanzania flag-XXL-anim.gif

BYE! BYE! MAGUFULI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI
 
Wale walinzi wa Magufuli wamejipanga kwenye jeneza kama walivyokuwa wanafanya akiwa hai
 
Sasa huyo ataenda mbinguni? Labda kama hizi hadithi za mbingu ziwe furahisha genge, lakini kama mbingu ipo kama tunavyosimuliwa, huyo mtu muovu haingii.
Lakini kwa mujibu wa maandiko kama atakuwa alitubu kabla ya mauti atasamehewa. Sasa hatujui kama alilifanya hilo lakini Mungu anajua.
 
Yoyote anayendeleza chuki dhidi ya Marehemu huwa ameshachukuliwa na roho ya Ibilisi, maana anapofariki Mwanadamu historia yake enzi ya uhai ni funzo kwa tuliobaki, Mwanadamu huzaliwa hajui kitu, hujifunza hapa duniani na mwisho anapopatwa mauti mwili hubaki haujui kitu chochote. Hivyo basi yatupasa tuliobaki kuwa na heshima ya Mazishi na kujifunza mema aliyoyafanya Marehemu yale mabaya alipokosea ni kama nasi tunavyokosea kila siku katika harakati za kazi za kibinadamu..Njia ni ileile huwezi jua pengine kesho ndio zamu yako..
Mungu awape wepesi walioguswa na Msiba huu.
R.I.P (H.E) Dr.JP MAGUFULI we believe GLORY of our Father in Heaven will stay with your SOUL forever..Amen
 
Ameshawasili eneo la tukio. Tutegemee Injili na Neno la Mungu safi lisilogoshiwa.

NB: Nondo zote zipo kwenye hiyo BRIFKESIView attachment 1729878
Hii picha (akiwa amevaa barakoa) inatuma ujumbe mzito wa watawala.

Viongozi wetu (hasa wa serikali) waache viburi. Tunaweza kujikuta kwenye hii awamu ya tano tunaongozwa na marais hata wanne kama tutaendelea kudharau UVIKO19.

Hii mikusanyiko ya kuaga tu ni tatizo. Sio ni kama kuna sensitivity yoyote ya kujaribu kuipunguza, kuiepuka au kuchukua tahadhari. Tunajali? Wacha tufe tu.
 
Yoyote anayendeleza chuki dhidi ya Marehemu huwa ameshachukuliwa na roho ya Ibilisi, maana anapofariki Mwanadamu historia yake enzi ya uhai ni funzo kwa tuliobaki, Mwanadamu huzaliwa hajui kitu, hujifunza hapa duniani na mwisho anapopatwa mauti mwili hubaki haujui kitu chochote. Hivyo basi yatupasa tuliobaki kuwa na heshima ya Mazishi na kujifunza mema aliyoyafanya Marehemu yale mabaya alipokosea ni kama nasi tunavyokosea kila siku katika harakati za kazi za kibinadamu..Njia ni ileile huwezi jua pengine kesho ndio zamu yako..
Mungu awape wepesi walioguswa na Msiba huu.
R.I.P (H.E) Dr.JP MAGUFULI we believe GLORY of our Father in Heaven will stay with your SOUL forever..Amen
Quinine hajui atendalo!
 
Back
Top Bottom