Dar: Yaliyojiri kuagwa kwa Mwili wa Hayati Dkt. Jonh Magufuli Uwanja wa Uhuru

Dar: Yaliyojiri kuagwa kwa Mwili wa Hayati Dkt. Jonh Magufuli Uwanja wa Uhuru

Chadwick Boseman alipokufa nililia sana japo nilimjua tu kwa kupitia muvi. Ila Magu daah tmpaka leo nipo Kwenye dozi naamini Magufuli anaweza kufa na watu.
Nilivyoona uzi jf wa Tanzia moyo ulienda mbio mwili ukachemka siku nzima ya alhamis nilishindwa kuinuka/kutembea. Niliwekewa drip 3[emoji22]

The reason baada ya Nyerere ni magufuli pekee niliyemuamini, I like to be Loyal. I was Loyal to JPm
Mfate kaburini
 
Kwakweli, me namuomba madam president abadilishe DPP pia, huyu aliepo ni chanzo cha mrundikano wa cases nyingi mahakamani na pia akipenda amteue Prof. Mussa Asad kuwa Prime minister au Vice President.
Kwani Assad ni mwana chama wa Ccm?au katiba inasemaje?
 
Hawa Askari waliokula kiapo inakuaje wanapita mbele ya janeza tena wamevaa sare na kofia wanapita kama raia au askari asiye na sare wanamaanisha nini hivi hawajui kama wanaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu??

Yaani naona hadi vijana wa Skauti wanapiga salute halafu jitu limevaa combati au OG na kofia juu linapita kienyeji tena jingine lipo kwenye mstari wa askari wenzake wanaopiga salute. Pumbavu wanapitaje kama mbele ya mkuu kama mapimbi, wanataka lawama baadae

Hawa ndio baadae wanataka lawana

Hii Mikanda itaangaliwa baada ya tukio kupita nawashangaa sana

Wanapitaje bila bila kupiga salute kwa aliyekuwa AMIRI JESHI MKUU?
View attachment 1730051View attachment 1730052View attachment 1730053View attachment 1730054View attachment 1730055
 
Mama Samia naomba tenda zote ukishika madaraka usimpe mhindi wala mwarabu hadi muda huu masaa kibao sijaona mhindi au mwarabu akimuaga Marehemu Magufuli.Akufaaye kwa dhiki ndie Rafiki naona wahindi na waarabu wametususia watanzania ngozi nyeusi.Sio kesi .Wanajitia watanzania wenzetu msibani hadi muda huu hawajatokea .Heri utoe tenda kwa waswahili kuliko hawa wahindi na waarabu

Mabalozi wa nje pia kuna aliyewaona kuaga? ili tumshauri vizuri Raisi wetu?
 
Kuna wimbi ulikua unaimba wakati Mapadri wanaaga mwili unaimba "Eeh Bwana unifaadhili mimi"
Mwenye kuujua anipatie jina au link please 🙏
Daah this song made 😢😢😭😭😭
 
Naamin nchi yetu ina misingi imara na tumepata Jembe jipya lenye makali zaid ya aliyepita,Rais wetu mpya atatuongoza vyema na atakuwa bora pia!

TUMUOMBEE DUA MAMA YETU RAIS WETU SAMIA SULUHU HASSAN HAKIKA ATATUVUSHA!
View attachment 1730126
 
Tumshukuru sana Mungu kwa zawadi ya uhai wa John Pombe Joseph Magufuli kwa nchi yetu. Ametutoa pagumu sana, ametuthubitishia yaliyoambiwa hayawezekani yanawezekana kwa vitendo.

Ametuachia viongozi makini aliowapika kuwa wazalendo kama yeye mwenyewe na ameacha wananchi wengi walio maskini wakiwa na cha kujivunia kwa nchi yao.

Ameiheshimisha Tanzania duniani kote kwa kuondoa uhuru wa bendera na kurudisha misingi ya uhuru halisi.

Ametuachia serikali makini chini ya aliyekua msaidizi wake makini Rais Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wote.

Ametuachia jamhuri ya muungano wa Tanzania iliyo imara, bunge imara, mahakama imara na jeshi imara.

Tumuombe Rais wetu Samia Suluhu Hassan aendeleze yale waliyoyaanza pamoja, na Mungu aendelee kumjaza hekma, ampe afya ya mwili, roho na akili katika kulitumikia taifa hili.

Rest well our hero President John Pombe Magufuli 💔😭🙏
 
Back
Top Bottom