Daraja jipya la Selander lakamilika, Kufunguliwa Desemba 27, 2021

Daraja jipya la Selander lakamilika, Kufunguliwa Desemba 27, 2021

All Credit to the Late JOHN POMBE MAGUFULI, jamaa alibana pesa ila tulijionea kwa macho pesa zikitengeneza na kuboresha miundombinu…

Aendelee kupumzika kwa Amani na kwa heshima yake ningependekeza liitwe Magufuli Bridge…
Mkopo huo
 
Katika tathmini yako umezingatia fidia kwa majengo yatakayobomolewa? Mfano mwenge hadi posta mpya kuna mijengo ya laana pembezoni mwa barabara
 
Acheni chuki za kishamba idea ndio msingi wa mradi! Usimamizi ndio unafata
Kama hujui feasibility study ya huo mradi ilianza 2014. Na 2015 mwishoni kuingia 2016 ndo Wakorea walitoa hela za ujenzi wa hilo daraja

Sasa, 2018 lilianza kujengwa na 2021 limekamilika! Kwa nini sifa apewe mmoja tu?
 
... Mkuu, hoja yangu ni kwamba tungeweza kufanya makubwa na yenye impact zaidi kwa wananchi masikini kwa kutumia the same resources.
Hilo kwako ni dogo?? Hii nchi ni kubwa huwezi kuhudumia wote kwa wakati mmoja, na ndio maana Mwanza ni JIJI na SHINYANGA NI MANISPAA. maendeleo ni hatua, tujipongeze na tuache lawama ambazo hata serikali ingeamua watafune hizo pesa kupitia warsha usingeziona.
 
Kazi ya Jakaya....mipango yote,michoro,usanifu,pesa n.k alishamaliza JK. Angalia hii post ya mwezi March- 2015 JPM akiwa Waziri wa Ujenzi na Miundombinu

Mtahangaika sana kudiscredit kila alichofanya ila hamtaweza. Miaka mingine mitano mtaendelea kufungua miradi yake...oops miradi ya Jakaya
 
Kampuni ya kikorea GS E& C wamemaliza ujenzi wa Daraja jipya la Selander ..mradi huu mkubwa utafunguliwa tarehe 27 Dec 2021.

Hii ni hatua njema ya ukamilishaji wa miradi yetu kama ilivyo kwenye Ilani ya ccm ya mwaka 2020-2025.

Daraja hili lina urefu wa mita 670 Ni aina mpya ya daraja ambayo imechanganya sifa za daraja la mhimili na daraja lililokaa kwa kebo ili kuifanya iwe nyepesi. Mbinu hiyo huongeza uwezekano wa ujenzi na kiuchumi, kulingana na mjenzi.

Mradi huu ulikuwa sehemu ya mradi wa Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini, ambao ulitoa dola milioni 107 kwa ujenzi huo.

View attachment 2053095
Mradi huu ulikuwa sehemu ya mradi wa Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini, ambao ulitoa dola milioni 107 kwa ujenzi huo.[emoji3064][emoji15][emoji3064][emoji15][emoji3064][emoji15]kumbe hazikuwa fedha zetu za ndani
 
Pesa atoe mkorea, kujenga ajenge mkorea alafu hongera unatoa kwa magufuli
Ucheke na wewe.

Tatizo vichaa wengi wanamtafutia credit kwa nguvu zote ila anakosa.

Hilo daraja Magufuli hausiki kwa lolote. Hakuna hata sh 100 ya Tz imelala hapo.
 
Mtahangaika sana kudiscredit kila alichofanya ila hamtaweza. Miaka mingine mitano mtaendelea kufungua miradi yake...oops miradi ya Jakaya
Soma link mkuu. Historia ni ngumu kufutika hasa ya mitandaoni.
 
Back
Top Bottom