Daraja jipya la Selander lakamilika, Kufunguliwa Desemba 27, 2021

Daraja jipya la Selander lakamilika, Kufunguliwa Desemba 27, 2021

Pesa atoe mkorea, kujenga ajenge mkorea alafu hongera unatoa kwa magufuli
kwa kiasi kikubwa limeisha under JPM, mpe zake tano hata kama hukubaliani na siasa zake, miradi mingi tuu ya mabilioni imekufa kwa uongozi mbovu, be happy tumepata daraja zuri litapendezesha jiji na litasaidia kupunguza foleni for the next 100 years
 
Kampuni ya kikorea GS E& C wamemaliza ujenzi wa Daraja jipya la Selander. Mradi huu mkubwa utafunguliwa tarehe 27 Dec 2021.

Hii ni hatua njema ya ukamilishaji wa miradi yetu kama ilivyo kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Selander Bridge Mpya (GS E&C)
Mjenzi wa GS E&C kutoka Korea Kusini amekamilisha ujenzi wa daraja la New Selander nchini Tanzania.

Daraja jipya la Selander litafunguliwa rasmi kwa matumizi tarehe 27 Desemba.

Daraja hili lina urefu wa mita 670 Ni aina mpya ya daraja ambayo imechanganya sifa za daraja la mhimili na daraja lililokaa kwa kebo ili kuifanya iwe nyepesi. Mbinu hiyo huongeza uwezekano wa ujenzi na kiuchumi, kulingana na mjenzi.

Mradi huu ulikuwa sehemu ya mradi wa Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini, ambao ulitoa dola milioni 107 kwa ujenzi huo.

View attachment 2053660

#SSH
#PIM
#KMM
#Tanzaniamoja
#TeamBomberdier
Napendekeza na wao walipie kama sisi watu wa kigamboni haiwezekani vigogo wapite bure huku watu watu wa kawaida kulipishwa
 
All Credit to the Late JOHN POMBE MAGUFULI, jamaa alibana pesa ila tulijionea kwa macho pesa zikitengeneza na kuboresha miundombinu…

Aendelee kupumzika kwa Amani na kwa heshima yake ningependekeza liitwe Magufuli Bridge…
Hakubana Bali alidhurumu hela za watanzania ikiwemo mishahara, malimbikizo, madai na kutoza Kodi haramu na kuwambikia watu makosa ili walipe faini
 
Hapana lipo ombi maalum kutoka kwa wana mtandao wa Msoga.Wameamua litaitwa Mosses Nauye hakuna namna lazima tuwaenzi wazee wetu.
Huyo Nnaye kaifanyia kitu gani special nchi hii?
 
All Credit to the Late JOHN POMBE MAGUFULI, jamaa alibana pesa ila tulijionea kwa macho pesa zikitengeneza na kuboresha miundombinu…

Aendelee kupumzika kwa Amani na kwa heshima yake ningependekeza liitwe Magufuli Bridge…
Ni mkopo kutoka Korea ya kusini
 
Hili nilikuwa sina wasiwasi nilijua litaisha on time na kwa kiwango cha juu maana kulikuwa hakuna pua ya mswahili iliyogusa au kuona pesa za hiyo project, pesa ilitolewa na Mkorea na akalipwa contractor moja kwa moja na kazi ikasimamiwa na mkorea 100%, model iliyotumika ni sumu kwa mafisadi, Congratulations to the late President JPM
Model iliyotumika inawanufaishaje wazawa?!
 
Model iliyotumika inawanufaishaje wazawa?!
Daraja limekamilika ndio muhimu na hatujaibiwa kama kawaida na usijifanye huelewi wapigaji wangepewa nafasi ya kulisimamia chance kubwa lisingekamilika, nina uhakika wafanyakazi wengi walikuwa watanzania na wamejifunza mengi tuu
 
Kampuni ya kikorea GS E& C wamemaliza ujenzi wa Daraja jipya la Selander. Mradi huu mkubwa utafunguliwa tarehe 27 Dec 2021.

Hii ni hatua njema ya ukamilishaji wa miradi yetu kama ilivyo kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Selander Bridge Mpya (GS E&C)
Mjenzi wa GS E&C kutoka Korea Kusini amekamilisha ujenzi wa daraja la New Selander nchini Tanzania.

Daraja jipya la Selander litafunguliwa rasmi kwa matumizi tarehe 27 Desemba.

Daraja hili lina urefu wa mita 670 Ni aina mpya ya daraja ambayo imechanganya sifa za daraja la mhimili na daraja lililokaa kwa kebo ili kuifanya iwe nyepesi. Mbinu hiyo huongeza uwezekano wa ujenzi na kiuchumi, kulingana na mjenzi.

Mradi huu ulikuwa sehemu ya mradi wa Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini, ambao ulitoa dola milioni 107 kwa ujenzi huo.

View attachment 2053660

#SSH
#PIM
#KMM
#Tanzaniamoja
#TeamBomberdier
Bwana Mjuaji umeacha umesahau hashtag ya #JPM

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom