Daraja la Wami liitwe Samia na Flyover ya Kurasini iitwe Mwinyi

Afanye mwingine aitwe mwingine.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sawa mkuu, siku njema.

: Lakini siku nyingine jitahidi kutumia lugha zenye staha kwa watu usio wafahamu.
Mkuu wewe unachukia Nini daraja likiitwa kwa jina la Rais wa Sasa? Mi sikufahamu ila tambua mi mkubwa wako huko ulipo,
 
Majina ya watu kwa madaraja ama majumba husaidia nini? ukifanya mazuri utakumbukwa tu si lazima uwe kwa daraja.
 
Hivi Tanzania watu wanaostahili kuenziwa ni wana siasa peke yao? Hasa kutoka chama tawala.

Amandla...
 
Kwanini mgawanye nchi kwa majina yenu? Kwani ikiitwa daraja la Wami kuna shida gani? Au kuna shida ikiitwa daraja la Kurasini? Yaani wananchi tukatwe tozo tujenge daraja afu from no where iitwe Samia?! Hii tabia naona inakithiri nchi hii. Mara Kijazi, mara Magufuli. Ya nini?
 
Na lile la kigongo-busisi tulipe jina la nani mkuu?
 
Bora ungeshauri apewe hilo daraja kuliko jina lake kulala porini kwenye mamba wanaomeza nondo za daraja na kusababisha lisikamilike.
 
Kwanini tusibadilishe jina la Jamhuri badala ya Tanzania tuiite Magufuli!!
Mmaonaje!!
Na mlima Kilimanjaro tuutafutie jina la mwanasiasa.

Vipi l uhusu Norongoro na Manyara!
Hakuna wanasiasa wenye hamu kupawa wakina (namesakes) wa Mali asili hizi ?

Alisikika mlevi moja akubwatuka maneno haya.
 
Mnadumaza history KWa vizazi vijavyo ,na majina yenu hayo, kwani ujenzi UKIFANYIKA Kuna kiongozi anatoa pesa mfukoni mwakwe ? Nyie vipi we unafikili mpaka jina mto wani lipo mnajua KWa nini waliita jina hilo , ipo siku Mtaita hata Mlima Kilimanjaro mlima wa jk, pinda, au Tulia mnapoelekea sipo 2025 mkiondoka majina haya ya kujipendekeza lazima yafutwe
 
Ni hatua mbaya tumefikia kama nchi. Zamani wanafunzi wanaenda shule ya Sekondari Magamba, Tosamaganga, Minaki, Weruweru, Ilboru, Kibaha, Mzumbe etc. Ghafla ikageuka Fredrick Sumatra secondary school, Benjamin Mkapa, Pius Msekea sekondari! Aiseee?l Hivi mtoto anafauluje kutoka shule inaitwa Benjamin Mkapa sec school? Au Fredrick Sumaye?! Ujinga. Sasa wanakuja na daraja la Kijazi, Magufu, sijui Mfugale flyover. Ni nini hii?! Tulipe kodi sisi, majina watajwe wao? Bila Kodi yetu hizo structures zingejengwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…