Daraja linalounganisha Dodoma na Morogoro limevunjika, hakuna mawasiliano ya barabara

Hapo Abiria wa wanaotoka Mwanza washalala na Abiria wanaoenda mwanza kesho hasa kampuni ya Dar Lux washafeli maana gari inayotegemewa haitavuka.

Hivi hakuna njia mbadala hapa (siyo ya Iringa) kuchepuka hapo hata kama ya porini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inafanana Na Daraja La Mandera Handeni
Tofauti Hapo Magubike Hakuna Njia Nyingine
 
Sema ahsante Mungu. Huyo unaemshukutu ndo kaleta mvua ama?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora tupumzike,Mungu kasikia kilio chetu manake viongozi wa kitaifa wanatusumbuaga sana kwa kutuweka mifoleni ya muda mrefu wakitumiaga njia hii kutoka huko mji mkuu,ikibidi hali iwe hvyo hvyo kwa mwezi mzima mbele aisee.

Mara utasikia miving'ora yao tu ng'wiiiiiii ng'wiiiiiiiiii
 
Halijaondoka na gari hilo daraja? Hivi hakuna kesi ya kujibu mkandarasi kanjanja hapo kweli?

Daraja gani lisilokuwa na beam? Lilikuwepo tu hapo likielea hewani kama paa la nyumba ya matope!

Kama hakuna ajali iliyopatikana hapo, kweli Mungu ni mkuu kaepushia mabalaa waja wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninawapa pole wasafiri wote waliokwama, ila mkandarasi wa hilo daraja alizingua daraja gani umejaa udongo tu ndiyo maana limekatika maana maji yalisababisha mmomonyoko ukaondoa udongo wote ikawa rahisi kukatika
 
Wakati mvua zikiendelea kunyesha barabara ya dodoma imekatika kabisa eneo la kiegeya hivyo kusababisha kukwama abiria na mizigo kukwama.

Hii ni hatari sana kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa letu ikizingatiwa kuwa Dodama ndiyo makao makuu ya taifa letu.

Nadhani sasa ATCL waongeze idadi ya ndege ili ziweze kuwasaidia wenzetu ambao watakuwa na uwezo wa kupanda hizo ndege.

In God we Trust
 
Reactions: PNC
Hali ni mbaya sana maana sasa kwa magari makubwa wameahauriwa kupitia iringa to dodoma au dodoma to iringa to dsm.

In God we Trust
 
Mwanachuo Dodoma washamaliza Boom na mitihani imeisha watakufa na njaa.

Portfolio | 2020
Hawawezi kufa njaa,kwa wanaonda Dsm wanapita Mtera wanaingia Iringa kutokea hapo maisha yanaendelea. Ama laaaa wanabadili pa kwenda . Sema tu gharama ya maisha inaweza ongezeka kidogo kwa wasafiri waliokuwa wakitumia njia hiyo na bidhaa hali kadhalika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…