Daraja linalounganisha Dodoma na Morogoro limevunjika, hakuna mawasiliano ya barabara

Daraja linalounganisha Dodoma na Morogoro limevunjika, hakuna mawasiliano ya barabara

Hapo nawashauri wenye mabasi au gari ndogo za abiria watumie njia ifuatayo ili kurahisisha kufika Dodoma kutokea Morogoro.

Ukitokea Moro nenda mpaka Dumila then kata kushoto kuelekea Kilosa then unaenda mpaka kijiji kinaitwa Lumuma. Kutoka hapo Lumuma unaenda mpaka Kibaigwa then Dodoma mjini. Njia ni nzuri na inapitika japokuwa ni ya vumbi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi picha zina malengo maovu ya kuhujumu uchumi! Wahusika wakamatwe haraka!
 
Kama hiyo SGR nayo inajengewa vikaravati uchwara maeneo korofi ya Morogoro itabidi huyo msimamizi wa mradi anyongwe hao waturuki wakikabidhi reli.
 
Ni Mabeberu wametufanyia hii kina Pompeo, sasa tunawaweka orodha ya kuwanyima viza wakati wanakuja kutuletea msaada
 
status_me_status_IMG-20200303-WA0000.jpg
 
Hizi picha zina malengo maovu ya kuhujumu uchumi!

Wahusika wakamatwe haraka!
Usemavyo Ni Hakika
Habari Hii Haikutakiwa Picture
Naona Aliyepiga 😅😄😃😂😁😀😀Alikuwa Anataka Tuone Nini
 
digba sowey, Hii ni barabara kuu inayounganisha Makao Makuu mapya ya Nchi, Dodoma na Dar es Salaam; na zone nzima ya magharibi mwa TZ mpaka nchi kadhaa za jirani upande huo.

Tangazo la TANROADS lilipasa kuonyesha umuhimu na uzito wa tukio hili kwa wadau wa nchini na wa kanda nzima ya Africa kama ifuatavyo:

1. Location ya daraja/mto katika ramani ya TZ.

2. Distance (in miles/kilometers) kutoka DSM hadi lilipo daraja au mto. Distance toka Dodoma hadi hapo.

3. Ramani ionyeshe alternative routes zote za ku-connect Dodoma na DSM sio Iringa peke yake.

4. Distance za alternative routes pia kwa kilometers/miles na kiwango cha barabara, kama ni lami au sivyo.

5. Matengenezo yatakamilika kwa muda gani au njia hiyo itafunguliwa lini.

Taarifa ya aina hii inasaidia watumiaji wote wa barabara hii, wa ndani na nje ya nchi kujua mambo hayo muhimu kwa wasafiri na wasafirishaji ili wafanye mipango ya shughuli zao vizuri zaidi.
Na hiki (at least) ndicho anachotakiwa kufanya mtu mwenye hadhi ya Mtendaji Makuu wa TANROADS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom