Darasa kwenye Shule ya Msingi Tella limeporomoka kutokana na uchakavu, masomo yanaende, viongozi wameitelekeza

Darasa kwenye Shule ya Msingi Tella limeporomoka kutokana na uchakavu, masomo yanaende, viongozi wameitelekeza

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Moja ya darasa la Shule ya Msingi Tella iliyopo katika Wilaya ya Hai hapa Mkoani kwetu Kilimanjaro limeporomoka kutokana na uchakavu wa majengo hayo ya shule lakini hakuna msaada tunaoupata kutoka kwa Viongozi wetu.

Wanafunzi wapo Shuleni wanaendelea na masomo kama kawaida huku tukiwa hatuna uhakika na usalama wa madarasa mengine.

Tumejaribu kumtafuta Mbunge wetu na Diwani wote hawapokei simu na hatujui nini kinaendelea, darasa liliporomoka wiki moja iliyopita lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika.

Wanafunzi wanaendelea kusoma katika madarasa mengine, hivi kweli ingekuwa ni Watoto wao hao Wanasiasa wangeendelea kuwa kimya kama hivi?

Shule hii yenye Wanafunzi zaidi ya 250 nimeona pia kuna madarasa yamefungwa hayatumiki kutokana na uchakavu.

Wizara ya Elimu mkoa wapi au mnasubiri msikie Walimu na Wanafunzi wamekufa ndio mtakuja na kamera nyingiii, inatia hasira sana.

IMG-20240726-WA0016.jpg

IMG-20240726-WA0017.jpg

 
Maafa mabaya yangewakuta wangekuwa darasani lakini heri imepatikana walikua shuleni!
 
Uongozi wa shule hawakuona huo uchakavu?
Viongozi wa shule mara nyingi sana huwa siyo wataalamu kwenye masuala ya Building Survey Engineering.
Serikali inapaswa iwe na Mipango ya kufanya Building Survey Inspections za mara kwa mara kwenye Majengo yake, ili Kama itabainika kuwa Jengo fulani lina uchakavu basi lifanyiwe Matengenezo au ukarabati Mapema kabla halijafikia hatua mbaya kama hii ya kubomoka au kuporomoka. Routine Maintenance or Preventive maintenance is required for all governments' schools infrastructures.
 
Kwa sisi tulivyo, tutakarabati hilo lililo bomoka na mengine tutayaacha mpaka nayo yaanguke.
 
Mbowe hawezi kukubali aibu jimboni kwake, atajenga chaap
 
Hizo shule watajenga wahisani, hela ya ndani ni ya kununua magari tu. Tumeupgrade magari ya mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya nchi nzima.

View attachment 3053279
Cc: CCM na mlaaniwe na Samia wenu milele..Watoto wana nusurika kufa Rais ananunua gari la KUNYEA kweli??Kwa CCM mavi ya Raisi ni bora kuliko uhai wa binadamu...?..:eti kuliko kujinyea yeye kwenye chupi?
 
Huyu mama hovyo sana.hera za kujenga shule hazipo lakini za kununua magari ya milioni miasita Moja anapata.
 
Back
Top Bottom