Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Moja ya darasa la Shule ya Msingi Tella iliyopo katika Wilaya ya Hai hapa Mkoani kwetu Kilimanjaro limeporomoka kutokana na uchakavu wa majengo hayo ya shule lakini hakuna msaada tunaoupata kutoka kwa Viongozi wetu.
Wanafunzi wapo Shuleni wanaendelea na masomo kama kawaida huku tukiwa hatuna uhakika na usalama wa madarasa mengine.
Tumejaribu kumtafuta Mbunge wetu na Diwani wote hawapokei simu na hatujui nini kinaendelea, darasa liliporomoka wiki moja iliyopita lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika.
Wanafunzi wanaendelea kusoma katika madarasa mengine, hivi kweli ingekuwa ni Watoto wao hao Wanasiasa wangeendelea kuwa kimya kama hivi?
Shule hii yenye Wanafunzi zaidi ya 250 nimeona pia kuna madarasa yamefungwa hayatumiki kutokana na uchakavu.
Wizara ya Elimu mkoa wapi au mnasubiri msikie Walimu na Wanafunzi wamekufa ndio mtakuja na kamera nyingiii, inatia hasira sana.