Nina mashaka na huyo anayejiita nabii, kama ameonyeshwa na Mungu kuwa Dar Es salaam inaenda kuadhibiwa, yeye kama nabii wajibu wake ni upi?
Nabii Yona aliambiwa na Mungu kuwa mji wa Ninawi Mungu atatoa hukumu juu yake,
Kabla ya hiyo hukumu kutolewa, Mungu alimtuma Mtumishi wake Yona aende Ninawi akawahubirie waakazi juu ya mpango wa Mungu, pamoja na ugumu wa Yona awali,
baada ya shinikizo la Mungu, Yona alienda kuhubiri, na aliuzunguka mji wote kuuelezea wasipotubu nini kitatokea,
Hakuwaambia uzeni mali zenu kisha hameni Ninawi, nendeni mjini mwingine, hakufanya hivyo,
Lkn huyu anawaambia watu wauze nyumba zao, gari na mali zao kisha wahamie kuanzia kibaha,
Je ana viwanja vingi kule anataka apige hela?
Au mawakala wa kuuza viwanja wanamtumia?
Je yeye na Kibwetere au Makezi wa Kenya wanatofauti ipi?