DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Lisaa la tatu mtu unasubiri gari hapa gerezani... yaani kufupi mwendokasi ni ukishapanda ila kwa muda unaosubiri hadi kupanda ni bora uchukue daladala tu... Gaddemit
Pamoja na changamoto zilizopo za uchache wa Mabasi sidhani kama unaweza kukaa masaa matatu kituoni ukisubiri basi, tunazidi kusisitiza mnapokutana na changamoto kama hiyo pigeni simu ya Bure 0800110147 ili kupata msaada wa haraka, taarifa kwetu ni muhimu sana ili kuona kama kuna uzembe mahala watu wachukuliwe hatua, lengo la usafiri huu sio kuwaletea adha wasafiri bali kuwarahisishia namna ya kutoka eneo moja kwenda lingine.
 
Acha siasa wewe, acha siasa,
 
Habari. Mi Nina malalamiko . Inakuwaje walinzi wenu WA pale kituo cha kimara wanasumbua abiria kw kuwakatalia kuingia na mizigo ikiwa wanajua kabis ni route ya kwenda Magufuli terminal kwa hiyo watu kuw na mizigo ni lazim sbb wanaend mikoani . Kuna mlinz mmoj Mzee flan alinipa stress kw kunizuia na mzigo WAngu nisipande basi la kwnda Magufuli kw sbb ya mzigo WAngu tena ni wakawaida Tu nimeubeba nimeufunga kwnye koroba akidai ni mkubw hivyo nirudi nikadai ela yangu ya tiketi nikapande daladala. Kumbuka Gerezani walinirusu nikapanda bila shida yeyeote Ile cha ajab pale kimara nimezuiwa kupanda ili niendelee na Safar Yang ya kwnd Magufuli. Kama ni hivyo ni Bora mubadilishe hio ruti wapen daladala sbb watu wakisfir lazm wawe na mizigo na UDART pekee Nd wanaruhusiw kufik mpka nje ya geti la Magufuli na wala sio daladala. Munapasw kupokea mizigo ya watu tofaut na apo wapeni wengn hio ruti . Over
 
Shida kubwa kituo cha Temboni Kimara ni lazima utoe pesa sadaka asb ndo uingie kwenye basi
 
Pole sana kwa changamoto iliyokukuta wakati mwingine ni suala la uelewa tu ndiomaana wa gerezani walikuruhusu, kuna utaratibu wa baadhi ya mizigo mikubwa kwa umbo na ile ambayo ni hatarishi kupakiwa ndani ya Mabasi, kwa sasa tunaandaa utaratibu kama wa uwanja wa ndege mizigo itakuwa ikipimwa kama uko kwenye kilo zinazoruhusiwa hakuna shida ila kama utakuwa umezidi itabidi uelekezwe cha kufanya , wakati mwingine ukipata changamoto kama hiyo piga namba yetu ya huduma kwa wateja ambayo ni ya BURE 0800110147 utasaidiwa kwa uharaka zaidi.
 
Ajira za wanaofanya usafi ztakosekana mkuu
 
Nauliza: Kwa kuwa mradi wa mwendokasi wa Mbagala-Magomeni karibu unamalizika mbona pale Kigogo bado kujengwa kituo?
Pia bado kipande cha Msimbazi Centre hadi Kigogo duara.
 
Nauliza: Kwa kuwa mradi wa mwendokasi wa Mbagala-Magomeni karibu unamalizika mbona pale Kigogo bado kujengwa kituo?
Pia bado kipande cha Msimbazi Centre hadi Kigogo duara.
Vipande ulivyovitaja vitafikiwa muda sio mrefu na kukamilika kwa wakati kabla ya mwaka huu kuisha, tuvute subra wakati mkandarasi anakamilisha kazi.
 
Vipande ulivyovitaja vitafikiwa muda sio mrefu na kukamilika kwa wakati kabla ya mwaka huu kuisha, tuvute subra wakati mkandarasi anakamilisha kazi.
Yani ni siasa mtindo mmoja. Bora tungekuwa Niger, tusingeremba siasa zikizidi
 
Je haya mnayoambiwa mnayafanyia kazi?, au kazi yenu kuomba maoni tu ili muonekane mna huduma Kwa wateja.
 
DART, DART, DART nimewaita 3 times.

1. Kwanini gari zetu ni mbaya mno ndani na hata nje je inamaana mmeshindwa kutangaza tenda ili kupatika kampuni kwaajili ya kuzifanyia maintenance gar zenu?

2. Gari zinaharibika mnazipaki jangwani mpaka zinakufa kabisa huku mjini kati uhaba wa gari unazidi kuongezeka jitafakarini.

3. Kwanini siku hizi hakuna Express mfano Kimara - Kibaha, Kimara - Kariakoo/Posta/Morocco maana hii simama yenu kila baada ya 200m inakera sana.

4. Kwanini mnapaki gari nyingine nzima tu hapa kimara na wakati abiria tunapata shida kugombania gari, kukanyagana bila sababu na wakati gari zipo?

5. Njia ya Kibaha mnajua dhahiri asubuhi na jioni hua inakua na abiria wengi kwanini mnaleta vipisi vya bus hamuoni kua nyie ndo mnaleta foleni kubwa na wakati mna ARTICULATED BUS?
 
Swali GUMU SANA [emoji1787][emoji1787]
Hakuna suala gumu kwetu kazi yetu ni kuhakikisha tunatoa huduma bora ya usafiri wa umma katika jiji la dar es salaam hususan kwenye maeneo ambako ushoroba wetu umepita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…