DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

1. Kuna vile vibao vya kuonesha gari inaenda wapi kwanini vinaandikwa kwa mkono ilihali haya magari yanakuja na system nzuri ya maandishi ya ki electroniki? havipendezi na vinakaa kama uchafu. Kama mmeshaharibu zile system naomba watafute wachoraji wazuri wa vibao wachore vya kupendeza

2. Ubovu wa viti na milango ni aibu naomba vifanyiwe kazi

3. Utaratibu wa kupanda mabasi uwe wa mistari kwenye kila kituo

4. Waongeze magari kwenye routr zote hususan mida ya jioni na asubuhi

5. Naomba msijaze sana abiria kwenye mabasi ni hatari kwa afya zetu na inanchangia uchakavu kwa haya magari. Mwanzoni mlikuwa hamruhusu watu kukaa mlangoni sasa hivi hata milango kufunga inakuwa tabu!
 
Madereva WENU na wale wafanyakazi wanapakizana na kushushana sehemu yeyote!

Tafadhali msifanye msaada shusheni vituo rasmi unless ni dharura kweli!!!!
 
Tentative dates za ujio wa magari mapya na matumizi ya kadi ji lini?
 
Ni lini mtaanza rasmi route ya mbagala hali ni mbaya Sana ya foleni, tafadhalini Kama inawezekana basi na ianze jkama dharula kwa kuwa hali ni mbaya
 
DART waambie madereva wenu kama hawataki kupakia abiria basi wakayapark kwenye Yard yenu jangwani na msilete kwenye vituo ,inakuwaje abiria wapo kibao wanasubiri gari ,linakuja linashusha abiria halafu linaenda pembeni linapark na si moja magari hata 6 yamepark halafu abairia wameshonana ,hivi wanaelewa maana ya mwendokasi? Hiyo miradi ya serikali ni ya kutoa huduma na si biashara maana tunakatwa kodi nyingi sizizo na kichwa wala miguu kwa ajili ya kuwezesha huduma kama hizo.
 
Hivi hayo magari hayajarudisha hela mchukue mapya?

Kuna Gari zimeshakaa kupitiliza
 
Hivi baada ya kutoa gharama za uendeshaji huwa mnapata faida kweli?

Maana sioni mambo matatu muhimu mkiyafanyia kazi.

1. Usafi ndani ya Magari na vituo vyenu.

2. Ununuzi wa Magari mapya na ukarabati wa yaliyopo.

3. Ukarabati wa miundombinu yenu.
 
Ni lini mtaanza rasmi route ya mbagala hali ni mbaya Sana ya foleni, tafadhalini Kama inawezekana basi na ianze jkama dharula kwa kuwa hali ni mbaya
Mwezi Oktoba mkandarasi anatukabidhi mradi ukiwa umekamilika baada ya hapo tutatoa taarifa ya lini wananchi wa Mbagala wategemee kuanza kwa huduma.
 
Back
Top Bottom