DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Mbona hipo tu ya kutosha, km 40 kwa dk 15 au 20 ukiwa na town hiace, sasa hapo unataka mwendo kasi ipi? Km 80 kwa saa 1 unataka mwendo kasi ya namna gani?
Barabara gani hiyo unazungumzia mkuu??
Ambayo unasema inatoa destiny ya 40 kilometres / 15 minuits ndani ya Mwanza jiji??
 
Kwa hapa kivukoni sa hv kama lisaa naona kuna mgomo wa madereva
 
Mbagala mbagala mbagala! ni lini mtaanza hii route hali si njema ndugu zetu tunataabika mno jamani.
 
Oktoba hii tunakabidhiwa miundombinu ikiwa imekamilika kabisa, baada ya hapo utasikia kutoka kwetu kuwa ni lini tutaanza huduma endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ikiwemo JF.

Jambo jema. Msikawie
 
Oktoba hii tunakabidhiwa miundombinu ikiwa imekamilika kabisa, baada ya hapo utasikia kutoka kwetu kuwa ni lini tutaanza huduma endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ikiwemo JF.
Kipande pale Kigogo sambusa hadi Mbuyuni hakijaisha plus pale Vera hapajanyooka basically na Oktoba ndio hiyo inayoyoma
 
Tupeni siri, nasikia pale kigogo round about kwenda ilala boma kina mazinga ombwe ndio mana hamkigusi,siku zinaenda sasa mtafanyaje?
Nyumba y'a wafu Ile Nadhani kuna roho zinadai
 
Miradi wa Maktaba to Tegeta unaanza lini na itachukuwa muda gani?
 
Ushauri wangu ni kuunga kipande cha barabara kutoka kwa Azizi Ally mpaka Changombe, enjoy hili lina wakazi wengi na litahudumia wengi.
 
Miradi wa Maktaba to Tegeta unaanza lini na itachukuwa muda gani?
Mkandarasi ameshakabidjhiwa eneo la ujenzi na sasa ameanzakuandaa materials kwa ajili ya kuanza ujenzi mara moja, jana kama umefuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ya intsgram, facebook, na X(twitter) ya @dartmwendokasi utaona hata mfadhili Benki ya Dunia alikuwa saiti kuangalia maandalizi ya kuanza kwa ujenzi.
 
Habari njema hii, mmejipangaje kupunguza foleni wakati wa ujenzi maana hii njia inakuwaje na foleni sana hasa jioni
 
hivi mnajua leo mmezingua na hakuna taaarifa mliyotoa abiria wanakaa zaidi ya saa moja kusubiri gari vituo vimejaa au mnafurahia hii hali

hivi mna SLA na wateja

katika huduma za hovyo tanzania yenu namba moja

nyie ni wapuuzi kuanzia viongozi wenu hadi bodi kama mnayo takribani miaka 10 hamjaleta hata basi moja hivi mmnaakili kweli

huu mradi nadhani utakua wa kigogo hamuwezi kuwa jeuri na kutesa watu asubuhi watu wanachelewa kazini
jioni watu wanachelewa nyumbani

mimi nimepoteza takribani elfu ishirini kwenye kadi zenu hadi leo sijarudishiwa lakini je ni lini mtaanzisha hii huduma au bado mnao upumbavu na utapeli

hivi mtaweza mbagala
watu wa kimara na mbezi ni wapole je mtawaweza wakurungwa wa mbagala

toka miaka karibia kumi huduma zinazidi kuzorota hakuna ubunifu wa kustua hakuna kuongeza hata gari
mnaanzisha route gari unasubiri nusu saa hadi lisaa

sioni hata mantiki ya kuweka huu uzi ni upuuzi mtupu

nataka hela yangu takribani 20k mlinitapeli kwenye kadi wapuuzi nyie

sijui kwann mmeleta uzi wenu hapa wakati huduma ni mbovu mshauriwe nini ambacho mtatekeleza gari tu kuongeza mmeshindwa wewe unae operate huu uzi nawewe pia mpuuzi

jibu au msipojibu mtajua wenyewe mshanitapeli zaidi ya miaka mitatu kenge nyie basi boresheni huduma hakuna
 
Habari njema hii, mmejipangaje kupunguza foleni wakati wa ujenzi maana hii njia inakuwaje na foleni sana hasa jioni
njia mbadala zitaainishwa na mamlaka husika ili kupunguza msongamano, pia mkandarasi atakuwa anafanya kazi zaidi usiku pia kupunguza changamoto hiyo.
 
Ndugu DART Mwendokasi hiyo njia kuelekea Tegeta inaenda mpaka eneo gani patakapokuwa na kituo kikuu cha kuanzia safari?.
 
Naomba muweke tangazo hairuhusiwi Kula au kunywa ndani ya vituo vya mabasi ya mwendokasi na ndani ya mabasi na walinzi wenu wasiruhusu mtu anaekunywa au Kula kuingia...hii itawasaidia usafi na kutupunguzia kero abiria ...hasa wanafunzi wa shule wanapanda mabasi huku wanakula maembe na ice cream na kutupakaza ...na kuchafua mabasi ...hili wala hakihitaji hela ..ni mabango na walinzi kusimamia
Hii post ya The Boss ina zaidi ya miezi 3, pamoja na kwamba it cost nothing in terms of financial resources nina uhakika hakuna katazo kama hili lilikowekwa!
 
Back
Top Bottom