DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Ongezeni magari,hasa jioni na asbh mana kuna siku nimekaa gerezani tangu sa1 jion kuja kupata gari sa3.

Mnazingua sana,
 
View attachment 2625074
DART Tumeanzisha ukurasa huu rasmi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa lengo la kupata maoni, ushauri , mrejesho na hata malalamiko yanayohusu huduma zetu. Aidha tunawahakikishia watumiaji wa huduma zetu kuwa maoni, ushauri, malalamiko, Pamoja na hoja zenu juu ya huduma zetu yatafanyiwa kazi kwa uharaka na hatua stahiki zitachukuliwa ili kuboresha huduma.

Kwa kupata msaada wa haraka kuhusu huduma zetu unaweza kutupigia simu 0800110147 ni bure. Kuanzia saa 11 alfajiri hadi saa tano na nusu usiku

Pia unaweza kutufuatilia katika tovuti ya www.dart.go.tz na mitandao yetu ya kijamii ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka ya FACEBOOK, INSTAGRAM, TWITTER, LINKEDIN, YOUTUBE.

Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka

Anuani
S.L.P 724, 16103
Ubungo Maji, Morogoro Road
Dar es Salaam, Tanzania

Barua pepe: info@dart.go.tz.

#usafiri wa umma nadhifu

#mwendokasi app
Uendeshaji wa hovyo kabisa kuanzia viongozi mpaka wafanyakazi wa chini kwa sababu sio kama hamuoni au kusikia kero za abiria wenu vituoni.
Bado mna wa zamani sana kupangisha watu foleni hivyo mradi mkubwa hivyo mnakosaje hata IT au Technician ambaye atakuwa mbunifu wa kubuni vitu katika mradi ili abiria wasipate kero au wenzetu mna degree za vyeti na sio za ubongo wa kuchanganua kero za abiria kwa haraka
Au tuseme kazi za kubebana na mnabeba vitu visivyo na kichwa wala miguu
 
Ushauri kwenu wakubwa ,ikiwezekana muwaambie wananchi baadhi ya vituo asubuhi muda fulani hadi muda fulani havitakuwa na huduma ,mmejimilikisha huduma ambayo kuna muda hamuwezi kukidhi mahitaji ya wateja hii sio sawa, inafika hatua mtu anakaa kituoni hadi anaamua kutoka kwenye kituo ili aokoe kibaria chake kwa kucheleweshwa na mwendo kasi, kwanza hata mantiki yenyewe ya mwendo kasi haionekani kabisa , kituo cha baruti hadi abiria wakwenda mjini wanaenda kujazana korogwe maana baruti unakaa zaidi ya dakika 40 hakuna gari inayosimama ,tunayaangalia yakipita na kudoma mabango,"hili la kivukoni,gerezani moroco hii sio sawa, na sio kwamba hamna uwezo bali ni utaratibu mbovu tu, hakuna usimamizi mzuri
 
Dart iwe decentralized,kila wilaya ya dsm iwe na dart yake na kuisimamia yenyewe,pia mnatumia gharama kubwa sana kutengengeneza vituo,sielewi kwa nini kituo ambacho tunategemea mtu asuburi gari dk 5 tu unamjengea kama nyumba,mkiangalie hilo
Pia ni vyema mkajikita zaidi Katika upanuzi wa barabara,ziwe njia hata nne,Tumeona inawezekana wakati wa ujenzi wa barabara ya mwendokasi Pugu road,nafasi ipo ya kupanua barabara,tuache utamaduni wa kuwa na njia nyembamba,panueni njia kisha muintroduce road toll mkusanye hela
 
Nasikia zinaongezwa daladala 15, kwenye njia ya DART kuna ukweli hapo?
 
Nasikia zinaongezwa daladala 15, kwenye njia ya DART kuna ukweli hapo?
Hakuna ukweli katika jambo hilo, kwanza daladala uwezo wake ni mdogo katika kubeba abiria wengi, pili miundombinu ya vituo hairuhusu kushusha na kupakia abiria kwani daladala ni fupi na hazijatengenezwa kwa ajili ya BRT.
 
Mi nilikuwa nashaur mabasi yote yawe na led light mbele na pembeni, led light zenye maandishi yanayobadilika yanayoelezea bus linatoka WAPI na linaenda WAPI ,maan dar inafikiwa na wagen wengi unakuta mtu kangia kwenye gar ndo anauliza hii gar inaenda wap kitu ambacho hakifai,kingine wale kama Askari sijui migambo waliopo pale wanatakiwa wakimuona mtu anazunguka zunguka wamfuate WA muulize unashida gan maana wao wanasubir Waulizwe unakuta kuna kunautaratibu WA folen mgen hajui anaona tu watu wamesimama kumbe wako kwenye folen we utashangaa Tu gar ikija wanageukiana,sasa Kwa mgen unakuta hajui chochote kinachoendelea unakuta kazagaa Tu lakin wale Askari wangekuwa wanamuwahi kumuliza wangemsaidia na kumwelezea utaratibu
 
Mbona wakati mradi unaanza zilikuwepo,pia ndani ya basi kulikua na pa ya kueleza gari linatoka wapi kwenda wapi na kila kituo kilikua kinatangazwa sema waafrika hasa wabongo ni waharibifu zaidi kuliko kutunza na kuboresha.
 
Mwendokasi wa mbagara gerezani utaanza lini? Mana taarifa mliyotoa ulitarajiwa uanze mwezi huu wa 10,sasa tuna siku 6 tu tumalize mwezi.
 
Mbona wakati mradi unaanza zilikuwepo,pia ndani ya basi kulikua na pa ya kueleza gari linatoka wapi kwenda wapi na kila kituo kilikua kinatangazwa sema waafrika hasa wabongo ni waharibifu zaidi kuliko kutunza na kuboresha.
Ndo shida warudishe na waweke mfumo WA kumentaini wakijua tuko AFRIKA na siyo ulaya
 
Ndo shida warudishe na waweke mfumo WA kumentaini wakijua tuko AFRIKA na siyo ulaya

Wanachojua ni kukusanya mapato na wala sio kutumia hayo makusanyo kuboresha,bali kuboresha matumbo yao,huu mradi umeingiwa na siasa uchwara ndio mana hauwezi kuja kuendelea zaidi ya kuendelea kuharibikiwa.
 
Ndo shida warudishe na waweke mfumo WA kumentaini wakijua tuko AFRIKA na siyo ulaya
maintenance my a55, gari likizingua tu,
utalikuta pale Jangwani limelazwa, na ndiyo mwisho wake huo

wakati mradi unaanza LED kubwa (GEREZANI-KIVUKONI, etc) kabisa ambazo zina scroll kulia-kwenda-kushoto zilikuwepo kwa windshield kwa juu
 
Mimi nahitaji kujua iwapo naweza kodi mwendokasi iwe inakuja kunichukua na kunirudhisha home kila siku iitwayo leo
 
maintenance my a55, gari likizingua tu,
utalikuta pale Jangwani limelazwa, na ndiyo mwisho wake huo

wakati mradi unaanza LED kubwa (GEREZANI-KIVUKONI, etc) kabisa ambazo zina scroll kulia-kwenda-kushoto zilikuwepo kwa windshield kwa juu
Zinatakiwa ziwe kwenye gar kabisa maana mtu anaweza pandia uko katikati
 
Back
Top Bottom