DART Special Thread: Tunaomba Maoni Ushauri, Malalamiko, Pongezi na Mapendekezo kuhusu Mabasi ya Mwendokasi

Tuwachane na hili shirika la umma, apewe tajiri mmoja aendeshe hii kampuni, kwisha kazi.

Hakuna cha umma kitachoendelea nchi hii. Shirika hili libinafsishwe tu.

Tumeanza toka kwa Nyerere huko, hakuna shirika la umma la usafiri lililobaki salama, mpaka leo hii.

Tulirithi DMT tumeiuwa, tukkaifanya UDA tumeiuwa, umekuja huu utumbo wa DAET tumeuuwa.

Kwanini tunarudia makosa yaleyale? Libinafsishwe 100%, serikali ingoje kodi tu.
 
swali la kwanza kwa Dart. 1.hivi mnajua idadi halisi ya watu wanatakiwa wapande gari zenu??2. Tunajenga miundombinu ya barabara why magari hatuongezi???3.mnashindwa kuboresha Mazingira ya vituo vyenu hasa mbezi to kimara mvua ikinyesha ni hatari

Niseme tu huduma imewashinda! Mabasi ni machache! Tafuteni Mbia wa kuendesha naye hiyo Huduma.
Usafiri wa Kutoka Kariakoo/Kivukoni-Kimara,Mbezi ni shida nyakati za Jioni ni shida.
Usafiri wa kutoka Mbezi-Kivukoni/Kariakoo,Kimara-Kariakoo/Kivukoni ni shida wakati wa asubuhi.
 
Swali wako wapi Dart wenyewe waje waseme
 
Hakuna taarifa iliyoeleza kuwa usafiri utaanza mwezi huu wa kumi isipokuwa kulikuwa na taarifa za mradi kukabidhiwa serikalini baada ya mkandarasi kumaliza ujenzi.
DART Mwendokasi hivi ni kwanini hiyo ruti ya mbagala haikamiliki na kuanza kazi? Maana kwa mwaka 2022 ilipofika msimu wa sabasaba mlianzisha safari lengo ilikua kupeleka watu sabsaba , na mwaka huu pia mkaleta mbwembwe zilezile msimu wa sabasaba, msimu ukiisha kimya

Kwanini hii ruti haikamiliki?
 
Kukamilika kwa ruti kuna maanisha , mosi barabara na miundombinu mingine iwe imekamilika kwa asilimia mia moja na kukabidhiwa, hii inajumuisha pia vituo taa za kuongozea magari, taa za barabarani vituo mlishi n.k. , sambamba na hilo awe amepatikana mtoa huduma mwenye uwezo wa kuwa na idadi ya Mabasi yaliyokusudiwa, kwa upande wa Mbagala mtoa huduma huyo atatakiwa kuwa na na uwezo wa kuleta Mabasi 750 kwa wakati mmoja,. Kwa sasa serikali iko kwenye hatua za kukamilisha upatikanaji wa mtoa huduma huyo na muda sio mrefu tutawapa mrejesho wa kinachoendelea.
 
Wazee wa poor planning, mabasi 750 halafu yawe yanalala ziwa jangwani?

Nyinyi Dart na serikali wote majipu
 
Mabasi 750 ila yanayoingia mzigoni 50 ayo mia700 yanabaki ktk karatasi
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
DART kubalini mmeshindwa kutoa huduma za usafirishaji kwa sababu watu wanasubiri basi kituoni saa 2. Mnaleta basi 1 kila baada ya saa 2 abiria wamechanganyikiwa wameshachelewa kazini wanataka kuvunjana miguu mlangoni na wanaingia bila kukaguliwa ticket mnakosa mapato kwa sababu ya ujinga wenu. Abiria wanagombania mwendokasi utafikiri wako Mbagala kwenye daladala. Hebu jirekebisheni au kama mmeshindwa kutoa huduma tafuteni mtoa huduma mwingine anayejiweza.
 
Uchache wa Mabasi ndio unasababisha adha hii ,lakini maelekezo ya serikali ni kutafuta mtoa huduma mwingine ambaye atashindana na huyu wa sasa ili kuboresha huduma, maelekezo hayo yanafanyiwa kazi na baada ya muda mfupi mtaona matokeo.
 
Hiki unachoongelea kipo katika utekelezaji wa muda gani nikimaanisha timeframe.
Si kwamba nafundiha namana ya kujibu swali ila.hili ni suala la.kiutemdahi umelijibu kisiasa siasa. Anachohitaji mwananchi ni mabasi yapo ya kutosha na huduma iliyo bora kuliko hapa ilivyo.
Yaani kampuni ina wasomi walioshika nafasi hizo mnashindwa na mtu mwenye daladala kumi?
 
Wazee wa poor planning, mabasi 750 halafu yawe yanalala ziwa jangwani?

Nyinyi Dart na serikali wote majipu
kutokujua mambo unaonekana hamna kitu kichwani depot ya mabasi ya mbagala ipo mbagala huko huko haiusiani na jangwani mabasi yatalala mbagala kingine cha kukusaidia soma ujue kati ya DART na UDART kuna tofauti gani

DART hamiliki mabasi ni mmiliki wa miundombinu sema anafelishwa na mtoa huduma, UDART akifeli mabasi yakiharibika lawama zote kwa DART sababu ni wakala wa serikali wa mabasi yaendayo haraka

kingne DART kumuwajibisha UDART ambae ni mtoa huduma pia inakuwa ngumu ingawa ndio kampa mkataba wa kutoa huduma za mabasi sababu ni kampuni ya serikali asilimia 85 ya share zote ni za msajili wa hazina apo mambo yanakua magumu serikali kumuwajibisha serikali
 
DART kubalini mmeshindwa kutoa huduma za usafirishaji kwa sababu watu wanasubiri basi kituoni saa 2. Mnaleta basi 1 kila baada ya saa 2 abiria wamechanganyikiwa wameshachelewa kazini wanataka kuvunjana miguu mlangoni na wanaingia bila kukaguliwa ticket mnakosa mapato kwa sababu ya ujinga wenu. Abiria wanagombania mwendokasi utafikiri wako Mbagala kwenye daladala. Hebu jirekebisheni au kama mmeshindwa kutoa huduma tafuteni mtoa huduma mwingine anayejiweza.
msafirishaji ni UDART , DART hana hata mabasi ni msimamizi wa mtoa huduma kwa niaba ya serikali sema mambo yanakua magumu pale ambapo unakuta anaemsimamia mwenye mabasi pia ni kampuni ya serikali kwa asilimia 85 kumtoa kutafuta mtoa huduma mwingne inakua ngumu labda kumuongezea mtoa huduma mwendokasi kuendesha ni ngumu sana kuliko mnavyofikiria mapato yanaenda world bank kulipa mkopo private sector ikitaka kuweka mabasi yake kwenye barabari za BRT ni ngumu sababu atabaki hana kitu.

makusanyo kwa siku yalipe word bank
makusanyo yalipe TRA
makusanyo yalipe DART tozo ya huduma
apo unabak hauna kitu

DART toka inaanzishwa wakurugenzi zaidi ya 2 wameishatumbuliwa UDART pia wakurugenzi zaidi ya 2 wameishatumbuliwa lkn mambo ni yale yale
 
kutokujua mambo unaonekana hamna kitu kichwani depot ya mabasi ya mbagala ipo mbagala huko huko haiusiani na jangwani mabasi yatalala mbagala kingine cha kukusaidia soma ujue kati ya DART na UDART kuna tofauti gani

DART hamiliki mabasi ni mmiliki wa miundombinu sema anafelishwa na mtoa huduma, UDART akifeli mabasi yakiharibika lawama zote kwa DART sababu ni wakala wa serikali wa mabasi yaendayo haraka

kingne DART kumuwajibisha UDART ambae ni mtoa huduma pia inakuwa ngumu ingawa ndio kampa mkataba wa kutoa huduma za mabasi sababu ni kampuni ya serikali asilimia 85 ya share zote ni za msajili wa hazina apo mambo yanakua magumu serikali kumuwajibisha serikali
Maelezo mazuri, maelezo hayo mazuri yametatua kero gani mpaka sasa mkuu kwa wananchi?
 
Wafanyakazi wenu hawawajali abiria kabila. Mfano mzuri ni mkaguzi wa tiketi wakati wa kuongia kwenye mabasi aliyeko kituo cha hospitali ya Muhimbili Upanga. Ni mwanamme wa makamo lakini ananyanyasa na kuwafokea hovyo abiria ambao baadhi ni wagonjwa. Anachafua taswira ya UDART
 
Back
Top Bottom