Ndio ilivyo unalipa 750/- pale Kibaha na tiketi haichanwi unakuja kimara unaendelea na safari ama kwenda gerezani au kivukoni!!! Swali kwani huwezi safiri kwa bei hiyo kutoka kivukoni/gerezani kwenda kibaha? Fanya utafiti kabla ya kuropoka!!!wewe bongo yoyo yaan utoke kibaha mpaka gerezani kwa 750 iyo mwendokasi ya wapi au ya china, nauli ya kibaha mpaka kimara ni 700 utoke kimara mpaka gerezan ni 750 jumla 1450
Mbagala nauli itakua bei gani? Ni saa 24 au saa ngap za kazi?
Suala la nauli na namna operations zitakavyokuwa mtatangaziwa baada ya route hiyo kuzinduliwa rasmiMbagala nauli itakua bei gani? Ni saa 24 au saa ngap za kazi?
Kwa sasa kazi zinaendelea kukamilishwa ikiwemo kumalizia ujenzi wa vituo vya kupandia na kushuklia abiria na kazi nyingine ndogo ndogo, muda ukifika wananchi watatangaziwa.Mwendokasi ya mbagala lini itaanza kufanya kazi??
Utaratibu upo tena tunautangaza na kuusisitiza kila siku, ukiwa na simu janja (smart phone) iwe ya android ama ya mfumo wa IOS unaweza kupakua Mwendokasi app kisha ukishakuwa nayo kwenye simu yako ni rahisi kuitumia kwa kufuata maelekezo machache, kwa namna programu hiyo ionavyofanya kazi angalia matangazo kwenye tovuti yetu www.dart.go.tz pia kupitia katika tovuti hiyo unaweza kuingia katika mitandao yetu ya kijamii ambayo pia ina maelezo ya Mwendokasi app.Ivi mna utaratibu wa mteja kununu tiketi kupitia simu yake ?
Hakuna mtu aliyekimbia tupo humu kwa saa 24 , ndiomaana tumeanzisha huu uzi kwa ajili ya kupata feedback ya namna mambo yetu yanavyokwenda.
Mwanza ipi unayoongelea wewe na zitapita wapi izo basi?Ngosha ukishashiba Sato ulale sio kuandika pumbaAsante kwa kuja.
Ni lini hayo mabasi mtayapeleka Mwanza pia ili wananchi wapate huduma ya usafiri..??
Sababu jiji la Mwanza limekua na tayari limechangamka na mkituletea hizo Bus zikaanzia route ya Kisesa, Igoma, Neshno, Buzuruga, Mabatini, Nata, Pepsi, Mkuyuni, Nyegezi, Buhongwa, Nyashishi hadi Usagara and Return.
Mkuu, mi nazungumzia mwanza ya daslam...Mwanza ipi unayoongelea wewe na zitapita wapi izo basi?Ngosha ukishashiba Sato ulale sio kuandika pumba
Aisee kweli kabisa,niliwahi shuka njiani kabla ya kufika nakoenda,nilikuwa nakosa hewa,nikaona Cha kufika nn, nikashuka!Wekeni hayo mabasi yenu AIC maana madirisha Huwa madogo na watu wanakuwa wengi sana jambo ambalo ni hatari.
Hafu kingine kwanini mabasi yenu mengine hupita vituoni matupu bila kusimama au kuchukua abiria hamuoni mnafanya biashara kichaa
MmmhhhhUtaratibu wa matumizi ya kadi ilisitishwa kutokana na changamoto mbalimbali za kiufundi, kwa sasa mpango wa kurudisha kadi unakaribia kukamilika na mtajulishwa matumizi yake yataanza lini na namna ya kupata kadi hizo.
Ebu sema neno mkuu...😂Mmmhhhh
Hili suala la upungufu wa mabasi siwaelewi kabisaaa, mabasi yamejaa yanrpaki tu getezani,kimara, kwanini?Kwa mujibu wa design tunatakiwa tuwe na basi kila baada ya dakika tano ,kwa sasa kwakua tuna upungufu wa mabasi ndiomaana hali haiko kama inavyotakiwa kuwa , lakini juhudi zinafanyika usiku na mchana na serikali yenu sikivu ya awamu ya tano kuhakikisha mabasi ya kutosha yanapatikana kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili kule Mbagala ambayo iko katika hatua za mwisho za umalishaji.
Nimeguna jibu lao naona wanamzingua tuEbu sema neno mkuu...😂
Hahahaaa! Kumbe unaikumbuka hii ishu, yule mtanesco kakomaa kweli kutaka namba watu tunamueleza vingine ye hatakiMkiwa active mtapata mengi sana. Ila msije mkaja na mambo ya wenzenu TANESCO ya kupewa changamoto walizonazo, wao badala ya kuhangaika na changamoto hizo, wanaanza mambo ya kutaka mtu aandike namba yake ya simu, anakoishi na jina lake kamili..!!!
Umesoma uzi kweli mkuu? Mbona namba ipoNAwwpongeza sana kwa hatua hii
Naomba DART muweke toll free number ya kupokea maoni na malalamiko ya wateja sisi.
Mkuu elezea kwanini watu wanakuwa kituoni halafu mabasi tunayaona yamepaki au yanatupita yakiwa matupu?Suala hili linafanyiwa kazi